12Ndipo watu wa Efraimu wakakusanywa pamoja na kuvuka kuelekea kaskazini, nao wakamwambia Yeftha: “Kwa nini ulivuka kupigana na wana wa Amoni, nawe hukutuita twende pamoja nawe?+ Nyumba yako tutaiteketeza juu yako kwa moto.”+
41 Na, tazama! watu wote wa Israeli walikuwa wakimjia mfalme, nao wakamwambia mfalme: “Kwa nini+ ndugu zetu watu wa Yuda walikuiba ili wamlete mfalme na nyumba yake na watu wote wa Daudi pamoja naye kuvuka Yordani?”+
10 Basi Amazia akawatenga, yaani, yale majeshi yaliyomjia kutoka Efraimu, ili waende kwao. Hata hivyo, hasira yao ikawaka sana juu ya Yuda, nao wakarudi kwao wakiwaka hasira.+