14 Kwa hiyo Hezekia mfalme wa Yuda akatuma ujumbe kwa mfalme wa Ashuru kule Lakishi, na kusema: “Nimetenda dhambi. Rudi nyuma, utoke juu yangu. Lolote utakalonitwika, nitalichukua.”+ Basi mfalme wa Ashuru akaweka juu ya Hezekia mfalme wa Yuda talanta+ 300 za fedha na talanta 30 za dhahabu.