47 Na tena watumishi wa mfalme wameingia ili kumtakia mema bwana wetu Mfalme Daudi, wakisema, ‘Mungu wako na alifanye jina la Sulemani kuwa na fahari kuliko jina lako, na akifanye kiti chake cha ufalme kuwa kikuu kuliko kiti chako cha ufalme!’+ Ndipo mfalme akainama juu ya kitanda.+