25 Basi, kwa kulinganisha na Absalomu, hakuna mwanamume aliyekuwa na sura nzuri+ sana katika Israeli yote kuweza kusifiwa sana hivyo. Hakuwa na kasoro yoyote, kuanzia wayo wa mguu wake mpaka kipaji cha kichwa chake.
14 Ndipo Yoabu akasema: “Acha nisijikawize hivi mbele yako!” Basi akachukua mkononi mwake mikuki midogo mitatu, akaichoma+ ndani ya moyo wa Absalomu alipokuwa bado hai+ katikati ya ule mti mkubwa.