14 Ndipo wanaume hao wakamwambia: “Nafsi zetu na zife badala yenu!+ Ikiwa hamtasema juu ya hii shughuli yetu, itatukia kwamba wakati Yehova atakapotupa nchi hii, sisi pia tutakutendea kwa fadhili zenye upendo na kwa uaminifu.”+
27 Baadaye wakuu wote wakamjia Yeremia na kuanza kumuuliza maswali. Yeye naye akawaambia kulingana na maneno hayo yote ambayo mfalme alikuwa ameamuru.+ Kwa hiyo wakanyamaza mbele yake, kwa maana habari hiyo haikusikiwa.