8 Na kwenye mpaka wa Yuda, kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi, mchango ambao ninyi mnapaswa kutoa unapaswa kuwa na upana wa mikono 25,000,+ na urefu kulingana na moja la yale mafungu kutoka mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi. Napo patakatifu patakuwa katikati yake.+