32 Basi akawaambia: “Nendeni!” Wakatoka na kwenda zao, wakaingia ndani ya wale nguruwe; na, tazama! kundi zima likatimua mbio, likaruka poromoko, likaingia baharini na kufa majini.+
13 Naye akawaruhusu. Ndipo wale roho wachafu wakatoka na kuingia ndani ya wale nguruwe; na lile kundi likatimua mbio, likaruka poromoko, likaingia baharini, wakiwa karibu elfu mbili, nao wakafa maji mmoja baada ya mwingine katika bahari.+