48 Na ikiwa mkaaji mgeni anakaa pamoja nawe akiwa mgeni naye atasherehekea pasaka kwa Yehova, kila mwanamume wa kwake na atahiriwe.+ Ndipo apate kukaribia ili kuisherehekea; na awe kama mwenyeji wa nchi. Bali mwanamume yeyote ambaye hajatahiriwa asipate kuila.