Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutoka 18:25, 26
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 25 Musa akachagua wanaume wanaostahili miongoni mwa Waisraeli wote na kuwaweka kuwa viongozi wa watu, kuwa wakuu wa maelfu, wakuu wa mamia, wakuu wa hamsini, na wakuu wa makumi. 26 Kwa hiyo waliamua kesi walizoletewa na watu. Kesi ngumu walimletea Musa,+ lakini waliamua kila kesi ndogo.

  • Hesabu 27:1-5
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 27 Kisha mabinti wa Selofehadi,+ mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, wa koo za Manase mwana wa Yosefu, wakaja. Mabinti hao waliitwa Mala, Noa, Hogla, Milka, na Tirsa. 2 Wakasimama mbele ya Musa, kuhani Eleazari, mbele ya wakuu,+ na mbele ya Waisraeli wote kwenye mlango wa hema la mkutano, wakasema: 3 “Baba yetu alikufa nyikani, lakini hakuwa miongoni mwa kikundi kilichojiunga na Kora kumpinga Yehova,+ bali alikufa kwa sababu ya dhambi yake mwenyewe naye hakuwa na mtoto yeyote wa kiume. 4 Kwa nini jina la baba yetu lipotee kutoka katika ukoo wake kwa sababu hakuwa na mtoto wa kiume? Tupe urithi miongoni mwa ndugu za baba yetu.” 5 Kwa hiyo Musa akawasilisha kesi yao mbele za Yehova.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki