-
Hesabu 23:13, 14Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
13 Balaki akamwambia: “Tafadhali, twende mahali pengine ambapo unaweza kuwaona. Utaona baadhi yao; hutawaona wote. Ukiwa huko walaani kwa niaba yangu.”+ 14 Kwa hiyo akampeleka kwenye uwanja wa Sofimu, juu ya Pisga,+ naye akajenga madhabahu saba na kutoa dhabihu ya ng’ombe dume mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.+
-
-
Hesabu 23:28-30Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
28 Basi Balaki akampeleka Balaamu juu ya Mlima Peori, unaoelekeana na Yeshimoni.*+ 29 Kisha Balaamu akamwambia Balaki: “Jenga madhabahu saba mahali hapa, nawe unitayarishie ng’ombe dume saba na kondoo dume saba.”+ 30 Kwa hiyo Balaki akafanya kama Balaamu alivyomwambia, naye akatoa dhabihu ya ng’ombe dume mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.
-