15 Basi nikawachukua viongozi wa makabila yenu, wanaume wenye hekima na uzoefu, na kuwaweka kuwa viongozi wenu, wakuu wa maelfu, wakuu wa mamia, wakuu wa hamsini, wakuu wa makumi, na maofisa wa makabila yenu.+
10 Ndipo Yoshua akawaamuru viongozi wa watu akisema, 11 “Piteni katika kambi yote na kuwaamuru watu hivi: ‘Tayarisheni vyakula, kwa sababu baada ya siku tatu mtavuka Mto Yordani ili kuingia na kuimiliki nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa.’”+