23 Wadudu wengine wote wenye mabawa wanaoishi katika makundi makubwa wenye miguu minne ni chukizo kwenu. 24 Wadudu hao watawafanya msiwe safi. Kila mtu anayegusa mizoga yao hatakuwa safi mpaka jioni.+
4 “‘Kitanda chochote anacholalia mtu anayetokwa na umajimaji hakitakuwa safi, na kitu chochote anachokalia hakitakuwa safi. 5 Mtu anayegusa kitanda cha mtu huyo ni lazima afue mavazi yake na kuoga kwenye maji, naye hatakuwa safi mpaka jioni.+