-
1 Mambo ya Nyakati 18:9-11Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
9 Mfalme Tou wa Hamathi aliposikia kwamba Daudi alikuwa amelishinda jeshi lote la Mfalme Hadadezeri+ wa Soba,+ 10 mara moja alimtuma Hadoramu mwana wake kwa Mfalme Daudi ili amjulie hali na kumpongeza kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda (kwa maana mara nyingi Hadadezeri alimshambulia Tou), na Hadoramu alimletea Daudi kila aina ya vitu vya dhahabu, fedha, na shaba. 11 Mfalme Daudi akavitakasa vitu hivyo ili viwe vya Yehova,+ pamoja na fedha na dhahabu aliyokuwa amechukua kutoka kwa mataifa yote: kutoka kwa Waedomu na Wamoabu, kutoka kwa Waamoni,+ Wafilisti,+ na Waamaleki.+
-