22 Basi Daudi akaondoka huko+ na kukimbilia katika pango la Adulamu.+ Ndugu zake na nyumba yote ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakashuka na kumfuata huko. 2 Na watu wote waliokuwa na shida na madeni na malalamishi wakakusanyika kwake, akawa kiongozi wao. Watu 400 hivi walikuwa pamoja naye.