-
1 Samweli 18:10, 11Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
10 Siku iliyofuata, roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamvamia Sauli,+ naye akaanza kutenda kwa njia ya ajabu* nyumbani, huku Daudi akipiga muziki kwa kinubi+ kama alivyofanya nyakati nyingine. Sauli alikuwa na mkuki mkononi,+ 11 basi akaurusha mkuki huo+ akisema hivi moyoni: ‘Nitampigilia Daudi ukutani!’ Lakini Daudi alimkwepa mara mbili.
-
-
1 Samweli 19:10Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
10 Sauli akajaribu kumpigilia Daudi ukutani kwa mkuki, lakini akamkwepa Sauli, na mkuki huo ukapenya ukutani. Daudi akakimbia na kutoroka usiku huo.
-