-
2 Samweli 4:5-8Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Rekabu na Baana, wana wa Rimoni Mbeerothi, walienda nyumbani kwa Ish-boshethi mchana wakati wa jua kali, alipokuwa akipumzika adhuhuri. 6 Wakaingia nyumbani mwake kana kwamba wamekuja kuchukua ngano, wakampiga tumboni; kisha Rekabu na Baana+ ndugu yake wakakimbia. 7 Walipoingia nyumbani, alikuwa amelala kitandani mwake katika chumba chake cha kulala, wakampiga na kumuua, kisha wakamkata kichwa. Halafu wakakichukua na kutembea usiku kucha kwenye barabara inayoenda Araba. 8 Wakamletea Daudi kichwa cha Ish-boshethi+ huko Hebroni na kumwambia mfalme: “Ndicho hiki kichwa cha Ish-boshethi mwana wa Sauli adui yako+ aliyetaka kukuua.+ Leo hii Yehova amekulipizia kisasi bwana wangu mfalme dhidi ya Sauli na wazao wake.”
-