-
2 Samweli 21:8-11Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
8 Basi mfalme akamchukua Armoni na Mefiboshethi, wana wawili ambao Rispa+ binti ya Aya alimzalia Sauli, na wana watano ambao Mikali*+ binti ya Sauli alimzalia Adrieli+ mwana wa Barzilai, Mmeholathi. 9 Daudi akawapa Wagibeoni wana hao, nao wakatundika maiti zao mlimani mbele za Yehova.+ Wana wote saba walikufa pamoja; waliuawa siku za kwanza za mavuno, mwanzoni mwa mavuno ya shayiri. 10 Kisha Rispa+ binti ya Aya akachukua gunia na kulitandika mwambani tangu mwanzo wa mavuno mpaka mvua kutoka mbinguni iliponyeshea maiti hizo; hakuruhusu ndege wa angani watue juu ya maiti hizo wakati wa mchana wala wanyama wa mwituni wazikaribie wakati wa usiku.
11 Daudi akaambiwa mambo ambayo Rispa binti ya Aya suria wa Sauli alikuwa amefanya.
-