Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Wafalme 7:51
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 51 Kwa hiyo Mfalme Sulemani akakamilisha kazi yote aliyopaswa kufanya kwa ajili ya nyumba ya Yehova. Kisha Sulemani akaingiza ndani vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa amevifanya kuwa vitakatifu,+ naye akaweka fedha, dhahabu, na vitu hivyo katika hazina za nyumba ya Yehova.+

  • 1 Wafalme 15:18
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 18 Ndipo Asa akachukua fedha yote na dhahabu iliyokuwa imebaki katika hazina za nyumba ya Yehova na hazina za nyumba ya* mfalme na kuwapa watumishi wake. Kisha Mfalme Asa akawatuma kwa Ben-hadadi mwana wa Tabrimoni mwana wa Hezioni, mfalme wa Siria,+ aliyekuwa akiishi Damasko, akamwambia:

  • 2 Wafalme 18:14, 15
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 14 Kwa hiyo Mfalme Hezekia wa Yuda akatuma ujumbe huu kwa mfalme wa Ashuru kule Lakishi: “Nimekosea. Ondokeni, msinishambulie, nami nitalipa chochote mtakachonitoza.” Mfalme wa Ashuru akamtoza Mfalme Hezekia wa Yuda faini ya talanta 300 za fedha* na talanta 30 za dhahabu. 15 Basi Hezekia akawapa fedha yote iliyokuwa katika nyumba ya Yehova na katika hazina za nyumba ya mfalme.*+

  • 2 Wafalme 24:12, 13
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 12 Mfalme Yehoyakini wa Yuda akatoka nje kwenda kukutana na mfalme wa Babiloni,+ akiwa pamoja na mama yake, watumishi wake, wakuu wake, na maofisa wa makao yake;+ na mfalme wa Babiloni akamchukua mateka katika mwaka wa nane wa utawala wake.+ 13 Kisha akachukua hazina zote za nyumba ya Yehova na hazina za nyumba ya mfalme.*+ Alivikata vipandevipande vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani mfalme wa Israeli alitengeneza katika hekalu la Yehova.+ Hilo lilitendeka kama Yehova alivyokuwa ametabiri.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki