-
Waamuzi 14:5, 6Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Basi Samsoni akaenda na baba yake na mama yake hadi Timna. Alipofika katika mashamba ya mizabibu ya Timna, simba* akamjia akinguruma. 6 Ndipo roho ya Yehova ikamtia nguvu,+ naye akampasua simba huyo vipande viwili, kama mtu anavyompasua mwanambuzi kwa mikono yake. Lakini hakumwambia baba yake au mama yake jambo alilofanya.
-
-
1 Samweli 17:36, 37Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
36 Mimi mtumishi wako nilimuua simba na dubu pia, na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amevitukana* vikosi vya Mungu aliye hai.”+ 37 Kisha Daudi akasema: “Yehova, aliyeniokoa kutoka katika makucha ya simba na ya dubu, ndiye atakayeniokoa kutoka mikononi mwa Mfilisti huyo.”+ Ndipo Sauli akamwambia Daudi: “Nenda, na Yehova awe pamoja nawe.”
-
-
2 Samweli 23:20-23Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
20 Benaya+ mwana wa Yehoyada alikuwa mwanamume jasiri* aliyefanya mambo mengi ya kishujaa kule Kabzeeli.+ Aliwaua wana wawili wa Arieli wa Moabu, naye aliingia ndani ya shimo la maji siku ya theluji na kumuua simba.+ 21 Alimuua pia mwanamume Mmisri aliyekuwa mkubwa isivyo kawaida. Ingawa Mmisri huyo alikuwa na mkuki mkononi, Benaya alikabiliana naye akiwa na fimbo, akamnyang’anya Mmisri huyo mkuki kutoka mkononi mwake na kumuua kwa mkuki wake mwenyewe. 22 Benaya mwana wa Yehoyada alifanya mambo hayo, naye alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu hodari. 23 Ingawa alikuwa mashuhuri hata kuliko wale 30, hakuwa shujaa kama wale watatu. Lakini Daudi alimweka kuwa kiongozi wa walinzi wake binafsi.
-