14 Na dhahabu iliyoletwa kwa Sulemani katika mwaka mmoja ilikuwa na uzito wa talanta 666 za dhahabu,+15 mbali na dhahabu iliyoletwa na wafanyabiashara wasafiri na pia faida kutoka kwa wauzaji wa bidhaa na kutoka kwa wafalme wote wa Uarabuni na magavana wa nchi.