36 Basi leo hii sisi ni watumwa+—naam, watumwa katika nchi ambayo uliwapa mababu zetu ili wale matunda yake na vitu vyake vyema. 37 Mazao yake mengi ni ya wafalme uliowafanya watutawale kwa sababu ya dhambi zetu.+ Wanatutawala wapendavyo na kuitendea mifugo yetu wapendavyo, tunateseka sana.