Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ayubu 38:8-11
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    •  8 Na ni nani aliyeizuia bahari nyuma ya milango+

      Ilipotoka kwa nguvu katika tumbo la uzazi,

       9 Nilipoivalisha mawingu

      Na kuifunika kwa* giza zito,

      10 Nilipoiwekea mpaka wangu

      Na kuweka makomeo yake na milango yake mahali pake,+

      11 Nami nikaiambia, ‘Unaweza kufika hapa, lakini usipite hapa;

      Hapa ndipo mawimbi yako ya kifahari yatakapokomea’?+

  • Zaburi 33:7
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    •  7 Huyakusanya maji ya bahari kana kwamba ni bwawa;+

      Huyaweka mawimbi makubwa ya maji katika maghala.

  • Zaburi 104:6-9
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    •  6 Uliifunika kwa vilindi vya maji kama kwa vazi.+

      Maji yalisimama juu ya milima.

       7 Kwa kemeo lako yalikimbia;+

      Kwa sauti ya mngurumo wako yalikimbia kwa wasiwasi

       8 —Milima ilipanda+ na mabonde yakashuka—

      Mahali ulipokusudia yawepo.

       9 Uliweka mpaka ambao hayapaswi kuvuka,+

      Ili yasiifunike dunia tena kamwe.

  • Yeremia 5:22
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 22 ‘Je, hamniogopi mimi?’ asema Yehova,

      ‘Je, hampaswi kutetemeka mbele zangu?

      Mimi ndiye niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari,

      Sheria inayodumu isiyoweza kukiukwa na bahari.

      Ingawa mawimbi yake yanasukasuka, hayawezi kushinda;

      Ingawa yananguruma, bado hayawezi kuvuka.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki