-
Yeremia 34:18-20Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
18 Na hivi ndivyo itakavyokuwa kwa watu waliolivunja agano langu kwa kutofuata maneno ya agano walilofanya mbele zangu walipomkata ndama vipande viwili na kupita kati ya vile vipande viwili,+ 19 yaani, wakuu wa Yuda, wakuu wa Yerusalemu, maofisa wa makao ya mfalme, makuhani, na watu wote wa nchi waliopita kati ya vile vipande viwili vya ndama: 20 Nitawatia mikononi mwa maadui wao na mikononi mwa wale wanaotaka kuwaua,* na maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani na cha wanyama wa dunia.+
-