-
Yeremia 39:5-7Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Lakini jeshi la Wakaldayo likawafuatia, nao wakamfikia Sedekia katika jangwa tambarare la Yeriko.+ Wakamkamata na kumleta kwa Mfalme Nebukadneza* wa Babiloni kule Ribla+ katika nchi ya Hamathi,+ ambako alimhukumu. 6 Mfalme wa Babiloni akaagiza wana wa Sedekia wachinjwe mbele ya macho yake kule Ribla, na mfalme wa Babiloni akaagiza wakuu wote wa Yuda wachinjwe.+ 7 Ndipo akayapofusha macho ya Sedekia, kisha akamfunga kwa pingu za shaba ili ampeleke Babiloni.+
-
-
Yeremia 52:9-11Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
9 Kisha wakamkamata mfalme na kumpeleka mpaka kwa mfalme wa Babiloni kule Ribla katika nchi ya Hamathi, naye akamhukumu. 10 Na mfalme wa Babiloni akawachinja wana wa Sedekia huku Sedekia akitazama, na pia akawachinja wakuu wote wa Yuda huko Ribla. 11 Kisha mfalme wa Babiloni akampofusha macho Sedekia,+ akamfunga kwa pingu za shaba, akampeleka Babiloni, na kumfunga gerezani mpaka siku aliyokufa.
-