3 Kisha Mfalme Nebukadneza akamwagiza Ashpenazi ofisa mkuu wa makao yake ya kifalme awalete baadhi ya Waisraeli,* kutia ndani wale wanaotoka katika uzao wa kifalme na wa watu mashuhuri.+
25 Mara moja Arioko akampeleka Danieli mbele ya mfalme na kumwambia: “Nimempata mwanamume fulani miongoni mwa watu waliohamishwa kutoka Yuda+ anayeweza kukueleza maana ya ndoto yako.”
13 Kwa hiyo Danieli akaletwa mbele ya mfalme. Mfalme akamuuliza Danieli: “Je, wewe ndiye Danieli, mmojawapo wa watu waliohamishwa na baba yangu mfalme kutoka Yuda?+