-
Marko 6:53-56Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
53 Walipovuka bahari, wakafika Genesareti na kutia nanga hapo karibu.+ 54 Lakini mara tu waliposhuka kutoka kwenye mashua, watu wakamtambua. 55 Wakakimbia katika eneo hilo lote na kuanza kuleta wagonjwa wakiwa kwenye vitanda* mahali waliposikia Yesu yuko. 56 Na kila mahali alipokwenda katika vijiji, majiji, au mashambani watu waliwaweka wagonjwa sokoni, na kumsihi waguse tu upindo wa vazi lake la nje.+ Na wote waliougusa wakapona.
-