-
Luka 13:6-9Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
6 Kisha akawaambia mfano huu: “Mtu fulani alikuwa na mtini uliopandwa katika shamba lake la mizabibu, akaenda kutafuta matunda kwenye mti huo lakini hakupata.+ 7 Ndipo akamwambia mtunza-mizabibu, ‘Kwa miaka mitatu nimekuwa nikija kutafuta matunda kwenye mtini huu, lakini sijayapata. Ukate! Kwa nini uendelee kuharibu ardhi?’ 8 Akamjibu, ‘Bwana, uache kwa mwaka mwingine mmoja niupalilie na kuutia mbolea. 9 Ukizaa matunda wakati ujao, vema; la sivyo, utaukata.’”+
-