Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Marko 12:13-17
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 13 Kisha wakawatuma baadhi ya Mafarisayo na wafuasi wa chama cha Herode ili wamnase kwa maneno yake.+ 14 Walipofika wakamwambia: “Mwalimu, tunajua wewe husema ukweli na hutafuti kibali cha yeyote, kwa maana huangalii sura ya nje ya mtu, bali unafundisha njia ya Mungu kupatana na kweli. Je, ni halali* au si halali kumlipa Kaisari kodi?* 15 Je, tunapaswa kulipa, au hatupaswi kulipa?” Akagundua unafiki wao, akawaambia: “Kwa nini mnanijaribu? Nileteeni dinari* niitazame.” 16 Wakaleta dinari moja, akawauliza: “Sura hii na maandishi haya ni ya nani?” Wakajibu: “Ni ya Kaisari.” 17 Ndipo Yesu akasema: “Mlipeni Kaisari vitu vya Kaisari,+ na Mungu vitu vya Mungu.”+ Nao wakashangazwa naye.

  • Luka 20:20-26
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 20 Baada ya kumtazama kwa makini, wakatuma watu waliowakodi kisiri wajifanye kuwa waadilifu ili wamnase Yesu kwa maneno yake+ na kumkabidhi kwa serikali na kwa mamlaka ya gavana. 21 Nao wakamuuliza: “Mwalimu, tunajua wewe husema na kufundisha kwa usahihi na huna ubaguzi, bali unafundisha njia ya Mungu kupatana na kweli: 22 Je, ni halali* au si halali kwetu kumlipa Kaisari kodi?”* 23 Lakini alitambua ujanja wao na kuwaambia: 24 “Nionyesheni dinari.* Ina sura na maandishi ya nani?” Wakajibu: “Kaisari.” 25 Akawaambia: “Basi mlipeni Kaisari+ vitu vya Kaisari, na Mungu vitu vya Mungu.”+ 26 Kwa hiyo, wakashindwa kumnasa kwa maneno yake mbele ya watu, nao wakanyamaza wakiwa wameshangazwa na jibu lake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki