-
Mathayo 8:30-33Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
30 Lakini kule mbali nao kulikuwa na kundi la nguruwe wengi wakila.+ 31 Kwa hiyo wale roho waovu wakaanza kumsihi: “Ukitufukuza, turuhusu tuingie katika lile kundi la nguruwe.”+ 32 Basi akawaambia: “Nendeni!” Ndipo wakatoka na kuingia ndani ya wale nguruwe, na tazama! kundi zima likatimua mbio, likaruka poromoko* likazama baharini na kufa maji. 33 Lakini wachungaji wakakimbia, na walipoingia jijini, wakasimulia mambo yote, kutia ndani habari kuhusu wale watu waliokuwa na roho waovu.
-
-
Luka 8:32-34Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
32 Sasa kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe+ waliokuwa wakila mlimani, basi wakamsihi awaruhusu waingie ndani ya nguruwe hao, naye akawaruhusu.+ 33 Ndipo wale roho waovu wakamtoka mtu huyo na kuingia ndani ya wale nguruwe, kisha lile kundi likatimua mbio, likaruka poromoko,* likazama ndani ya ziwa na kufa maji. 34 Wachungaji walipoona kilichotokea, wakakimbia na kupeleka habari hizo jijini na mashambani.
-