Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 21:33-41
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 33 “Sikilizeni mfano mwingine: Kulikuwa na mtu aliyemiliki shamba, akapanda shamba la mizabibu+ na kulizungushia ua, akachimba shinikizo la divai* ndani yake, akajenga mnara;+ kisha akalikodisha kwa wakulima, naye akasafiri kwenda ng’ambo.+ 34 Majira ya matunda yalipofika, akawatuma watumwa wake kwa wakulima ili wakachukue matunda yake. 35 Hata hivyo, wakulima hao wakawakamata wale watumwa, mmoja wakampiga, mwingine wakamuua, na mwingine wakampiga mawe.+ 36 Akawatuma tena watumwa wengine, wengi zaidi ya wale wa kwanza, lakini wakawatendea vivyo hivyo.+ 37 Mwishowe akamtuma mwana wake kwao, akisema, ‘Watamheshimu mwanangu.’ 38 Wakulima walipomwona yule mwana wakaambiana, ‘Huyu ndiye mrithi.+ Njooni tumuue ili tuuchukue urithi wake!’ 39 Kwa hiyo wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu na kumuua.+ 40 Basi, mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawatendea nini wakulima hao?” 41 Wakamwambia: “Kwa sababu ni waovu, atawaangamiza kabisa na kulikodisha shamba la mizabibu kwa wakulima wengine, ambao watampa matunda yatakapoiva.”

  • Luka 20:9-16
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 9 Yesu akaanza kuwaambia watu mfano huu: “Mtu fulani alipanda shamba la mizabibu+ akalikodisha kwa wakulima, kisha akasafiri kwenda ng’ambo, akakaa huko muda mrefu.+ 10 Majira yalipofika akamtuma mtumwa kwa wakulima ili wampe baadhi ya matunda ya shamba la mizabibu. Hata hivyo, wale wakulima wakampiga na kumfukuza mikono mitupu.+ 11 Lakini akamtuma mtumwa mwingine. Huyo pia wakampiga, wakamwaibisha,* na kumfukuza mikono mitupu. 12 Bado tena akamtuma wa tatu; huyo pia walimjeruhi na kumtupa nje. 13 Ndipo mwenye shamba la mizabibu akasema, ‘Nifanye nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa.+ Labda watamheshimu.’ 14 Wakulima walipomwona wakaambiana, ‘Huyu ndiye mrithi. Basi tumuue, ili urithi wake uwe wetu.’ 15 Wakamtupa nje ya shamba la mizabibu na kumuua.+ Kwa hiyo, mwenye shamba la mizabibu atawafanya nini? 16 Atakuja na kuwaua wakulima hao, kisha atawapa watu wengine shamba hilo la mizabibu.”

      Waliposikia hivyo wakasema: “Jambo hilo lisitukie kamwe!”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki