Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 9:3-8
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 3 Sasa baadhi ya waandishi wakaambiana: “Mtu huyu anakufuru.” 4 Yesu, akijua fikira zao, akasema: “Kwa nini mnawaza mambo maovu katika mioyo yenu?+ 5 Kwa mfano, ni jambo gani rahisi zaidi kusema, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Simama utembee’?+ 6 Hata hivyo, ili mjue kwamba Mwana wa binadamu ana mamlaka ya kusamehe dhambi duniani—” kisha akamwambia yule mtu aliyepooza: “Simama, chukua kitanda chako, uende nyumbani.”+ 7 Ndipo akasimama, akaenda nyumbani. 8 Umati ulipoona hivyo ukaogopa, nao wakamtukuza Mungu aliyewapa wanadamu mamlaka ya namna hiyo.

  • Luka 5:21-26
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 21 Ndipo waandishi na Mafarisayo wakaanza kujadiliana: “Huyu ni nani anayesema makufuru? Ni nani anayeweza kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?”+ 22 Lakini Yesu, akifahamu mawazo yao akawauliza: “Mnawaza nini katika mioyo yenu? 23 Ni jambo gani rahisi zaidi kusema, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Simama utembee’? 24 Lakini ili mjue kwamba Mwana wa binadamu ana mamlaka ya kusamehe dhambi duniani—” akamwambia yule mtu aliyepooza: “Ninakuambia, Simama, uchukue kitanda chako, uende nyumbani.”+ 25 Ndipo akasimama mbele yao, akachukua kitanda chake, akaenda nyumbani, akimtukuza Mungu. 26 Kisha wote wakashangaa wakaanza kumtukuza Mungu, wakastaajabu na kusema: “Leo tumeona mambo ya ajabu!”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki