-
Mathayo 12:24-29Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
24 Mafarisayo waliposikia jambo hilo wakasema: “Mtu huyu anawafukuza roho waovu kwa nguvu za Beelzebuli,* mtawala wa roho waovu.”+ 25 Akijua fikira zao, akawaambia: “Kila ufalme uliogawanyika dhidi yake wenyewe utaangamia, na kila jiji au nyumba iliyogawanyika dhidi yake yenyewe haitasimama. 26 Vivyo hivyo, ikiwa Shetani anamfukuza Shetani, amegawanyika dhidi yake mwenyewe; basi, ufalme wake utawezaje kusimama? 27 Zaidi ya hayo, ikiwa ninawafukuza roho waovu kupitia Beelzebuli, wana wenu wanawafukuza kupitia nani? Hiyo ndiyo sababu watakuwa waamuzi wenu. 28 Lakini ikiwa ninawafukuza roho waovu kupitia roho ya Mungu, kwa kweli Ufalme wa Mungu umewafikia ninyi ghafla.+ 29 Au yeyote anawezaje kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuchukua mali zake isipokuwa kwanza amfunge mtu huyo? Hapo ndipo anaweza kuipora nyumba yake.
-