-
Mathayo 12:24-30Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
24 Mafarisayo waliposikia jambo hilo wakasema: “Mtu huyu anawafukuza roho waovu kwa nguvu za Beelzebuli,* mtawala wa roho waovu.”+ 25 Akijua fikira zao, akawaambia: “Kila ufalme uliogawanyika dhidi yake wenyewe utaangamia, na kila jiji au nyumba iliyogawanyika dhidi yake yenyewe haitasimama. 26 Vivyo hivyo, ikiwa Shetani anamfukuza Shetani, amegawanyika dhidi yake mwenyewe; basi, ufalme wake utawezaje kusimama? 27 Zaidi ya hayo, ikiwa ninawafukuza roho waovu kupitia Beelzebuli, wana wenu wanawafukuza kupitia nani? Hiyo ndiyo sababu watakuwa waamuzi wenu. 28 Lakini ikiwa ninawafukuza roho waovu kupitia roho ya Mungu, kwa kweli Ufalme wa Mungu umewafikia ninyi ghafla.+ 29 Au yeyote anawezaje kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuchukua mali zake isipokuwa kwanza amfunge mtu huyo? Hapo ndipo anaweza kuipora nyumba yake. 30 Yeyote asiye upande wangu ananipinga, na yeyote asiyekusanya pamoja nami anatawanya.+
-
-
Marko 3:22-27Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
22 Pia, waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu walikuwa wakisema: “Ana Beelzebuli,* naye anawafukuza roho waovu kwa nguvu za mtawala wa roho waovu.”+ 23 Kisha akawaita na kuzungumza nao kwa mifano: “Shetani anawezaje kumfukuza Shetani? 24 Ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe, hauwezi kusimama;+ 25 na nyumba ikigawanyika dhidi yake yenyewe, haiwezi kusimama. 26 Pia, ikiwa Shetani anajipinga mwenyewe na amegawanyika, hawezi kusimama, bali ataangamia. 27 Kwa kweli, hakuna yeyote anayeweza kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuiba mali zake isipokuwa kwanza amfunge mtu huyo. Hapo ndipo atakapoweza kuipora nyumba yake.
-