Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 9:2
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 2 Na tazama! wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelala kwenye kitanda.* Alipoona imani yao, Yesu akamwambia yule mtu aliyepooza: “Jipe moyo mwanangu! Umesamehewa dhambi zako.”+

  • Marko 2:3-12
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 3 Wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne.+ 4 Lakini kwa sababu ya umati, hawakuweza kumleta moja kwa moja kwa Yesu, basi baada ya kutoboa sehemu ya paa lililokuwa juu ya Yesu, wakamteremsha yule mtu aliyepooza, akiwa amelala juu ya kitanda.* 5 Yesu alipoona imani yao,+ akamwambia yule mtu aliyepooza: “Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.”+ 6 Sasa baadhi ya waandishi waliokuwa wameketi hapo wakaanza kuwaza mioyoni mwao:+ 7 “Kwa nini mtu huyu anasema hivyo? Anakufuru. Ni nani anayeweza kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?”+ 8 Lakini mara moja Yesu akatambua rohoni mwake kwamba walikuwa wakiwaza hivyo, basi akawaambia: “Kwa nini mnawaza mambo hayo katika mioyo yenu?+ 9 Ni jambo gani rahisi zaidi, kumwambia mtu huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Simama, uchukue kitanda chako utembee’? 10 Lakini ili mjue kwamba Mwana wa binadamu+ ana mamlaka ya kusamehe dhambi duniani—”+ akamwambia yule mtu aliyepooza: 11 “Ninakuambia, Simama, chukua kitanda chako, uende nyumbani.” 12 Ndipo akasimama, na mara moja akachukua kitanda chake akatembea mbele yao wote na kwenda nje. Basi, wote wakashangaa, na kumtukuza Mungu wakisema: “Hatujawahi kamwe kuona jambo kama hilo.”+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki