Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 17:1-8
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 17 Siku sita baadaye, Yesu alienda pamoja na Petro, Yakobo na Yohana ndugu yake kwenye mlima mrefu wakiwa peke yao.+ 2 Sura yake ikageuka mbele yao; uso wake ukang’aa kama jua, na mavazi yake ya nje yakang’aa* kama nuru.+ 3 Tazama! wakaona Musa na Eliya wakizungumza na Yesu. 4 Ndipo Petro akamwambia Yesu: “Bwana, ni vizuri sisi tuwe hapa. Ukitaka, nitasimamisha mahema matatu hapa, moja lako, moja la Musa, na moja la Eliya.” 5 Alipokuwa bado akizungumza, tazama! wingu jangavu likawafunika, na tazama! sauti kutoka katika lile wingu ikasema: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa, ambaye nimemkubali.+ Msikilizeni.”+ 6 Wanafunzi waliposikia hilo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana. 7 Ndipo Yesu akawakaribia, akawagusa na kuwaambia: “Simameni. Msiogope.” 8 Walipotazama juu, hawakumwona mtu yeyote ila Yesu tu.

  • Marko 9:2-8
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 2 Siku sita baadaye Yesu akaenda pamoja na Petro, Yakobo, na Yohana kwenye mlima mrefu wakiwa peke yao. Sura yake ikageuka mbele yao;+ 3 mavazi yake ya nje yakaanza kumetameta, yakawa meupe kuliko vile mfuaji nguo yeyote duniani angeweza kuyasafisha. 4 Pia, wakaona Eliya na Musa, wakizungumza na Yesu. 5 Kisha Petro akamwambia Yesu: “Rabi, ni vizuri sisi tuwe hapa. Basi, tutasimamisha mahema matatu, moja lako, moja la Musa, na moja la Eliya.” 6 Kwa kweli, hakujua afanye nini, kwa maana walikuwa wameogopa sana. 7 Wingu likatokea na kuwafunika, na sauti+ ikasikika kutoka katika lile wingu ikisema: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa.+ Msikilizeni.”+ 8 Kisha ghafla wakatazama huku na huku na hawakumwona tena mtu yeyote isipokuwa Yesu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki