Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 17:1-8
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 17 Siku sita baadaye, Yesu alienda pamoja na Petro, Yakobo na Yohana ndugu yake kwenye mlima mrefu wakiwa peke yao.+ 2 Sura yake ikageuka mbele yao; uso wake ukang’aa kama jua, na mavazi yake ya nje yakang’aa* kama nuru.+ 3 Tazama! wakaona Musa na Eliya wakizungumza na Yesu. 4 Ndipo Petro akamwambia Yesu: “Bwana, ni vizuri sisi tuwe hapa. Ukitaka, nitasimamisha mahema matatu hapa, moja lako, moja la Musa, na moja la Eliya.” 5 Alipokuwa bado akizungumza, tazama! wingu jangavu likawafunika, na tazama! sauti kutoka katika lile wingu ikasema: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa, ambaye nimemkubali.+ Msikilizeni.”+ 6 Wanafunzi waliposikia hilo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana. 7 Ndipo Yesu akawakaribia, akawagusa na kuwaambia: “Simameni. Msiogope.” 8 Walipotazama juu, hawakumwona mtu yeyote ila Yesu tu.

  • Luka 9:28-36
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 28 Kwa hakika, karibu siku nane baada ya Yesu kusema maneno hayo, alienda mlimani na Petro, Yohana, na Yakobo ili kusali.+ 29 Alipokuwa akisali uso wake ukabadilika, mavazi yake yakawa meupe na kuanza kumetameta. 30 Na tazama! wanaume wawili walikuwa wakizungumza naye; walikuwa Musa na Eliya. 31 Walitokea wakiwa na utukufu na wakaanza kuongea kuhusu kuondoka kwake, ambako kungetimizwa huko Yerusalemu.+ 32 Petro na wenzake walikuwa wamelemewa na usingizi, lakini walipoamka kabisa waliuona utukufu wa Yesu+ na wanaume wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye. 33 Wale wanaume wawili walipokuwa wakiondoka, Petro akamwambia Yesu: “Mwalimu, ni vizuri sisi tuwe hapa. Basi, tutasimamisha mahema matatu, moja lako, moja la Musa, na moja la Eliya.” Hakujua alichokuwa akisema. 34 Lakini alipokuwa akisema mambo haya, wingu likatokea na kuanza kuwafunika. Walipokuwa wakifunikwa na wingu, wakaogopa. 35 Kisha sauti+ ikasikika katika lile wingu ikisema: “Huyu ni Mwanangu aliyechaguliwa.+ Msikilizeni.”+ 36 Walipokuwa wakisikia ile sauti, wakamwona Yesu akiwa peke yake. Lakini wakakaa kimya na katika siku hizo hawakumwambia mtu yeyote lolote kati ya mambo waliyoona.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki