15 Wakafika Yerusalemu. Akaingia hekaluni akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni, naye akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadili pesa na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa,+ 16 na hakumruhusu mtu yeyote apite hekaluni akiwa amebeba chombo.