-
Yohana 13:3-5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
3 Basi, Yesu akijua kwamba Baba alikuwa ameviweka vitu vyote mikononi mwake na kwamba alikuja kutoka kwa Mungu na alikuwa akienda kwa Mungu,+ 4 akasimama kutoka kwenye mlo wa jioni na kuyaweka kando mavazi yake ya nje. Naye akachukua taulo, akajifunga kiunoni.+ 5 Akatia maji kwenye beseni, akaanza kuiosha miguu ya wanafunzi na kuikausha kwa taulo aliyokuwa amejifunga kiunoni.
-