-
Mathayo 27:27-29Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
27 Ndipo wanajeshi wa gavana wakampeleka Yesu katika makao ya gavana, wakakusanya kikosi chote cha wanajeshi kumzunguka.+ 28 Wakamvua kanzu yake na kumvisha joho jekundu,+ 29 kisha wakasokota taji la miiba na kumvisha kichwani na kutia utete kwenye mkono wake wa kuume. Wakampigia magoti, wakamdhihaki wakisema: “Salamu,* ewe Mfalme wa Wayahudi!”
-