Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwanzo 41:40-46
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 40 Wewe binafsi utaisimamia nyumba yangu, na watu wangu wote watakutii kabisa.+ Nitakuwa tu mkuu kuliko wewe ninapotimiza jukumu langu nikiwa mfalme.”* 41 Kisha Farao akamwambia Yosefu: “Tazama, ninakuweka kuwa msimamizi wa nchi yote ya Misri.”+ 42 Halafu Farao akaivua pete yake ya muhuri kutoka kwenye mkono wake mwenyewe na kumvisha Yosefu mkononi, akamvisha pia mavazi ya kitani bora na mkufu wa dhahabu shingoni mwake. 43 Zaidi ya hayo, akampandisha katika gari lake la pili la heshima, na watu walikuwa wakimtangulia na kusema kwa sauti, “Avrekh!”* Kwa hiyo Farao akamweka kuwa msimamizi wa nchi yote ya Misri.

      44 Tena Farao akamwambia Yosefu: “Mimi ni Farao, lakini hakuna mtu anayepaswa kufanya jambo lolote* bila idhini yako katika nchi yote ya Misri.”+ 45 Kisha Farao akampa Yosefu jina Zafenath-panea, na pia akampa Asenathi+ binti ya Potifera kuhani wa Oni* awe mke wake. Naye Yosefu akaanza kuisimamia* nchi ya Misri.+ 46 Yosefu alikuwa na umri wa miaka 30+ alipoanza kumtumikia* Farao mfalme wa Misri.

      Kisha Yosefu akaondoka mbele ya Farao na kutembea katika nchi yote ya Misri.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki