5 Pesa, Uzito, Vipimo
Viwango vinavyofuata ni wastani unaotegemea ushuhuda wa Biblia na mavumbuzi ya vitu vya kale vilivyofukuliwa. Ulinganifu wote wa sasa ambao umetumiwa katika maandishi haya unapasa kuonwa kuwa ni makadirio. Vipimo viowevu na vikavu ni kulingana na vipimo vya Marekani (U.S.).
Ili kupata thamani ya sasa ya dhahabu au fedha, unahitaji kujua thamani ya hivi karibuni zaidi ya kila gramu moja na kuzidisha na hesabu ya gramu.
Katika maandishi ya Kigiriki kwenye Ufu 14:20; 21:16 vipimo vya umbali vimeonyeshwa kwa namna ya stadia. (Stadia moja ya Kiroma = 1⁄8 ya maili moja ya Kiroma au futi 625 za Kiroma; meta 185; futi 606.75 za Uingereza).
ORODHA YA PESA KULINGANA NA UZITO KATIKA MAANDIKO YA KIEBRANIA
Ulinganifu wa Sasa
Gera 1 = 1⁄20 ya shekeli = gramu 0.57
Beka 1 (nusu shekeli) = gera 10 = gramu 5.7
Shekeli 1 = beka 2 = gramu 11.4
Mina 1 (mane) = shekeli 50 = gramu 570
Talanta 1 = mina 60 = kilo 34.2
Dariki 1(ya Uajemi, dhahabu) = gramu 8.4
Dariki 1 (ya Uajemi, fedha)
(pia iliitwa shekeli) = gramu 5.60
ORODHA YA PESA ZA UGIRIKI NA ROMA KULINGANA NA UZITO KATIKA MAANDIKO YA KIGIRIKI
Ulinganifu wa Sasa
Leptoni 1 (ya Kiyahudi,
shaba au shaba nyeusi) = 1⁄2 ya kwadrani
Kwadrani 1 (ya Kiroma,
shaba au shaba nyeusi) = leptoni 2
Asi au asarioni 1
(ya Kiroma na ya
majimboni, shaba
au shaba nyeusi) = kwadrante 4
Dinari 1 (ya Kiroma, fedha) = asi 16 = gramu 3.85
Drakma 1 (ya Ugiriki, fedha) = gramu 3.40
Didrakma 1 (ya Ugiriki, fedha) = drakma 2 = gramu 6.80
Tetradrakma 1
(stateri ya fedha) = drakma 4 = gramu 13.6
Mina 1 = drakma 100 = gramu 340
Talanta 1
(dhahabu au fedha) = mina 60 = kilo 20.4
VIPIMO VIOWEVU (VYA MAJI-MAJI)
Logi 1 = 1⁄4 ya kabi = lita 0.31 = painti 0.66 (U.S.)
Kabi 1 = logi 4 = lita 1.22 = painti 2.58 (U.S.)
Hini 1 = kabi 3 = lita 3.67 = painti 7.75 (U.S.)
Bathi 1 = hini 6 = lita 22 = galoni 5.81 (U.S.)
Koria 1 = bathi 10 = lita 220 = galoni 58.1 (U.S.)
VIPIMO VIKAVU
Kabi 1 = logi 4 = lita 1.22 = painti 2.2 (U.S.)
Omeri 1 = kabi 1 4⁄5 = lita 2.2 = vibaba 2 (U.S.)
Sea 1 = omeri 3 1⁄3 = lita 7.33 = vibaba 6.66 (U.S.)
Efa 1 = sea 3 = lita 22 = vibaba 20 (U.S.)
Homeri 1 (kori) = efa 10 = lita 220 = vibaba 200 (U.S.)
VIPIMO VYA UREFU NA UPANA
Upana wa kidole 1 = 1⁄4 ya kiganja = sm 1.85 = inchi 0.72
Upana wa kiganja 1 = vidole 4 = sm 7.4 = inchi 2.9
Shubiri 1 = viganja 3 = sm 22.2 = inchi 8.75
Mkono 1 = shubiri 2 = sm 44.5 = inchi 17.5
Mkono mrefub 1 = viganja 7 = sm 51.8 = inchi 20.4
Utete 1 = mikono 6 = meta 2.67 = futi 8.75
Utete mrefu 1 = mikono mirefu 6 = meta 3.11 = futi 10.2
Pima 1 = meta 1.8 = futi 6
[Maelezo ya chini]
a Pia kipimo kikavu kilicholingana na homeri.