Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 5/8 uku. 31
  • Uamuzi Waongezea Haki za Wagonjwa?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uamuzi Waongezea Haki za Wagonjwa?
  • Amkeni!—1991
  • Habari Zinazolingana
  • Kulinda Salama Watoto Wenu na Matumizi Mabaya ya Damu
    Huduma Yetu ya Ufalme—1992
  • Kupigania Uhuru wa Kuabudu
    Ufalme wa Mungu Unatawala!
  • Hospitali— Wakati Wewe Ni Mgonjwa
    Amkeni!—1991
  • Vijana Wenye “Nguvu Ipitayo Iliyo ya Kawaida”
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 5/8 uku. 31

Uamuzi Waongezea Haki za Wagonjwa?

“HAKI ya mtu ya kuongoza mwili wake ni wazo ambalo limetambuliwa kwa muda mrefu na sheria ya kawaida,” alitaarifu Bw. Hakimu Mkuu Sydney Robins wa Mahakama ya Rufani ya Ontario, Canada. Lakini ni nini kilichochea suala hilo hapo awali?

Katika 1979 Bw. na Bi. Malette wa Quebec, Canada, walihusika katika msiba wa motokaa ambao uliua mume na kumwacha mke akiwa amejeruhiwa vibaya na akiwa bila fahamu. Alipokimbizwa hospitali, ilipatikana kwamba alikuwa na Medical Directive/Release Card, yenye kukataa waziwazi kutiwa damu mishipani kwa kutegemea sababu hususa za kidini. (Pia kuna hatari za kiafya zinazoshirikishwa na kutiwa damu mishipani.) Daktari aliyemtibu, akiamini kwamba hali yake ilikuwa ya hatari, alipuuza maagizo hayo na akajitwalia daraka la kumpa damu. Likiwa tokeo la hilo, Bi. Malette alishtaki daktari huyo na hospitali kwa ajili ya kushambulia na kuumiza na ubaguzi wa kidini. Katika mahakama ya kujaribia, alipewa ridhaa ya $20,000. Kesi hiyo ilikatwa rufani kwenye mahakama kuu zaidi ya Ontario, Mahakama ya Rufani.

Mojawapo hoja zilizorudiwa katika uamuzi wa Mahakama ya Rufani ya kuunga mkono Bi. Malette ulikuwa huu:

“Haki ya kukataa utibabu ni sehemu iliyorithiwa ya ukuu wa haki ya mgonjwa juu ya mwili wake. . . . Hata uhai uwe mtakatifu namna gani, maelezo ya kijamii yasiyopendelea yakubali kwamba sehemu fulani za maisha huchukuliwa kuwa za maana zaidi kuliko uhai wenyewe. Vichocheo hivyo vya viwango vya juu na vya kuheshimika vimetia mizizi katika jumuiya kwa muda mrefu, iwe ni kwa ajili ya uzalendo katika vita [au] kulinda uhai wa mwenzi wa ndoa, mwana au binti . . . Katao la utibabu kwa msingi wa kidini ni kiwango cha aina hiyo.”

Maoni ya mahakama ya rufani yaliendelea hivi: “Bila kujali maoni ya daktari, mgonjwa ndiye mwenye uamuzi wa kama atapewa utibabu huo. . . . Kama daktari angechukua hatua baada ya uamuzi wa kukataa matitabu hayo, angejibu kisheria kwa ajili ya mwenendo wake usioidhinishwa . . . Daktari hayuko huru kupuuza maagizo ya kimbele ya mgonjwa [kama vile Medical Directive/Release Card ambayo huchukuliwa na Mashahidi wa Yehova] wala hayuko huru kupuuza maagizo yanayotolewa wakati wa dharura.” Mahakama hiyo iliongeza kwamba “kutia damu mishipani Shahidi wa Yehova kinyume cha maagizo yake yanayokataza ingekuwa . . . kuvunja haki yake ya kuongoza mwili wake mwenyewe na kuonyesha kukosa heshima kwa thamani za kidini ambazo yeye amechagua kuishi maisha yake.”

Kisha hakimu mkuu huyo wa rufani alitokeza wazo lenye nguvu dhidi ya daktari aliyekuwa amedai kwamba kadi hiyo haikuwa na thamani yoyote katika dharura hiyo. “Mimi sikubali . . . kwamba kadi ya huyu Shahidi wa Yehova ni kikaratasi tu kisicho na maana. . . . Maagizo katika kadi ya huyu Shahidi wa Yehova yaliweka kizuizi halali juu ya utibabu wa dharura ambao angeweza kupewa Bi. Malette na yalikataza kutiwa damu mishipani. . . . Taarifa yake iliyoandikwa imekusudiwa waziwazi kuonyesha mapendezi yake anapokuwa hawezi kujisemea mwenyewe.”

Katika maneno yake ya kumalizia hakimu mkuu huyo alitoa wazo la akili kwamba Mashahidi wanapokataa kutiwa damu mishipani, “wanapaswa kujitwalia matokeo ya uamuzi wao. Wala wao au wenye kuwategemea hawawezi kusema baadaye kwamba kadi hiyo haikuwakilisha mapendezi yao ya kweli.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki