Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 5/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1991
  • Habari Zinazolingana
  • Biblia Inasema Nini Kuhusu Dinosa?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Namna Gani Kazi-Maisha za Kuwa Violezo vya Mapambo na Kufanya Mashindano ya Urembo?
    Amkeni!—1990
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 5/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Ubatizo Asanteni sana kwa ajili ya makala “Vijana Wauliza . . . Je! Nibatizwe?” (Aprili 8, 1991) Ule usiku kabla tu ya kupokea toleo hilo, nilisali kwa ajili ya msaada nijue kama nilikuwa tayari kubatizwa. Makala hiyo ilieleza niliyokuwa nikihisi hasa. Natazamia sana ubatizo wangu.

A.S., United States

Nilishukuru kwa ajili ya makala “Vijana Wauliza . . . Je! Nibatizwe?” (Aprili 8, 1991) Kisa cha Susana mwanzoni mwa makala hiyo kilifanya moyo wangu ujawe na hisia nyingi. Nilijiweka wakfu kwa Mungu nilipokuwa katika mwaka wangu wa sita wa shule ya msingi, na hilo lilinisaidia kweli kweli kubaki mwenye nguvu katika imani. Je! isingekuwa vizuri sana kama vijana wote Wakristo wangeonyesha ujitoaji ule ule kama yule towashi Mwethiopia na kuuliza, “Ni nini kinachonizuia nisibatizwe?”—Matendo 8:36.

M.A., Japan

Utafiti wa Kutumia Wanyama Nilithamini sana makala yenu. (Aprili 8, 1991) Nilijua kwamba majaribio hufanyiwa wanyama, lakini sikujua kamwe kwamba wao hutumiwa katika utengenezaji wa vitu vya kujipodoa, vya kusafisha nywele, na visafishaji! Nangojea kwa hamu wakati ambao matumizi hayo mabaya yatakoma.

R.M., Italia

Ulimwengu Bila Bunduki Makala zenu za karibuni juu ya bunduki (Novemba 8, 1990) ziliniudhi. Taarifa “bunduki zikidi, mifyatuko itazidi” ilikaziwa na mfululizo wa vielelezo na manukuu yanayopotoa hali iliyo halisi. Kwa kielelezo, mwataarifu kwamba Uswisi ina hesabu kubwa ya bunduki kwa wastani wa watu katika Ulaya. Lakini katika makala zenu hamtaji popote kwamba Uswisi pia ina mojawapo viwango vya chini vya uhalifu na uuaji katika ulimwengu! Kulaumu bunduki kwa ajili ya matatizo yanayosababishwa na watu waovu yaelekea ni kosa.

K.C., United States

Twathamini maelezo hayo. Maelezo fulani ya wazi yangelipasa kutolewa kuhusiana na baadhi ya tarakimu zenye kutokeza ubishi zaidi katika makala zetu. Hata hivyo, “Amkeni!” halikuwa likichukua msimamo juu ya suala la kisiasa la kudhibiti bunduki bali lilikuwa likitetea “ulimwengu bila bunduki” wa wakati ujao chini ya Ufalme wa Mungu. Hadi wakati huo, Wakristo wanaongozwa na kanuni kwenye Isaya 2:4 na Mathayo 26:52.—MHARIRI.

Mimba za Utineja Lazima niwapongeze kwa sababu ya ushauri mzuri sana mliotoa katika makala yenu juu ya mimba za utineja. (Oktoba 8, 1990) Nilipokuwa na miaka 16, nilizaa binti yangu. Ingawa baba yake alikuwa na nia ya kunioa, familia yangu ilinishauri kwamba nilikuwa mchanga mno. Familia yangu ilinisaidia hadi nilipoolewa baadaye. Miaka mingi baadaye nilianza kujifunza Biblia pamoja na Mashahidi wa Yehova. Leo binti yangu hutumikia akiwa mhudumu wa wakati wote. Nafurahi sana sikutoa mimba wala kuingia katika ndoa ya mapema!

L.B., United States

Ilikatisha tumaini kusoma kwamba ingawa wazazi wa kulea mtoto ambaye hawakuzaa waweza kuandalia mtoto vizuri zaidi kimwili, upendo na shauku hutolewa kwa kufaa zaidi na wazazi wake wa asili. Nikiwa mama mwenye kulea mtoto asiye wangu, mimi nina pendeleo zuri sana la kulea mwana wetu mdogo katika njia za Yehova.

C.R., Jamhuri ya Muungano wa Ujerumani

Twasikitika iwapo makala hii ilisababisha kutokuelewa fulani. Wazazi wengi waliolea watoto ambao hawakuwazaa hufanya kazi nzuri sana ya kuwapa watoto wao tegemezo na upendo unaohitajiwa. Hata hivyo, makala hii ilikuwa ikizungumzia uwezekano wa kwamba mtoto anayepelekwa akalelewe na wengine huenda asilelewe kulingana na viwango vya Kikristo. Ikiwa ndivyo, msichana ambaye hajaolewa hapaswi kukata kauli kwamba hana kitu cha kumpa mtoto wake. Yeye aweza kumlea kulingana na viwango vya Biblia na kumwonyesha upendo wa kweli—jambo ambalo ni la maana zaidi ya faida za kiuchumi.—MHARIRI.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki