Imani Yao Yahamisha Milima
LIKIWA na kichwa hicho gazeti la kila siku Buenos Aires Crónica, la Desemba 7, 1990, liliripoti mkusanyiko wa Mashahidi wa Yehova uliokuwa ukifanywa katika stediamu za soka za River Plate na Vélez Sarsfield. Kwa kweli, ni imani thabiti iliyowasukuma wajumbe wa kigeni karibu 6,000 kutoka nchi zaidi ya 20 kusafiri mwendo wote hadi Argentina ili kujiunga na makumi ya maelfu ya ndugu zao Waargentina kwenye mkusanyiko wao wa “Lugha Iliyo Safi.” Hesabu hii ilitia ndani makundi kadhaa ya Mashahidi Wakorea. Wajumbe wa kigeni walitoka Uingereza, Kanada, Chile, Japani, Uhispania, United States (kutia ndani Alaska), na nchi nyinginezo nyingi. Ni nini kiliwasukuma? Tamaa yao ya kuunga mkono mkusanyiko wa kimataifa wa pili katika Argentina.
Kuwekwa Wakfu kwa Betheli Mpya
Lakini matendo makuu ya imani yalitokea kabla ya wakati wa mkusanyiko. Katika Oktoba ofisi ya tawi jipya ya Argentina ya Asociación de los Testigos de Jehová liliwekwa wakfu na Theodore Jaracz msemaji mwenye kuzuru wa Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova. Makao hayo mapya yalikuwa yamejengwa na wafanya kazi 259 wa kimataifa na 690 wa Argentina wenye kujitolea. Betheli, au “Nyumba ya Mungu,” iliyo katika sehemu yenye mistari ya miti ya Buenos Aires, ina vyumba vya makao 129 na chumba cha kulia cha watu 300. Kukiwa na Mashahidi 84,000 katika Argentina na uwezekano wa ongezeko zaidi, hakuna shaka kwamba jengo hili jipya la ofisi litajazwa karibuni.
“Mashahidi wa Yehova Wenye Lugha Safi”
Kichwa “Lugha Iliyo Safi” cha mkusanyiko huo wa kimataifa kilivutia wengi, kutia na wawakilishi wa habari. Crónica ilielekeza kwenye kichwa kilicho juu na kunukuu ufafanuzi wa “Lugha Iliyo Safi” kama ilivyotolewa na msemaji: “Uelewevu sahihi wa kweli kuhusu Mungu na makusudi yake kwa dunia na mwanadamu, kama ulivyo katika Biblia . . . Mtu ajifunzapo kuisema lugha iliyo safi, basi njia yake ya kufikiri, usemi wake, na mwenendo wake huwa katika kutambua Mungu kuwa Mungu wa pekee wa kweli.”
Buenos Aires, ambalo ni jiji lililoenea huku na huku la watu zaidi ya milioni kumi, lilijulishwa sana juu ya mkusanyiko wenye kufanyika humo. Katika kipindi cha siku sita, ule muda wa kawaida wa sekunde 40 za redio na TV za matumbuizo na matangazo ya biashara zenye kuidhinishwa na sheria, ulijilisha tukio hilo kwa umma. Programu ya Jumamosi ilivutia waandishi wa habari kwa ubatizo wa Mashahidi wapya. Vikiwa vyaonekana vyema na watazamaji, vidimbwi 3 viliwekwa katika kila pembe ya viwanja vyote viwili, lakini hata vidimbwi 12 havikutosha kutimiza ubatizo kwa wakati kabla ya programu ya alasiri. Kwa hiyo vidimbwi katika River Plate vilihamishwa mahali ambapo havingeonekana. Katika River plate, 1,363 walibatizwa na katika Vélez Sarsfield, 748, kukiweko jumla ya 2,111! Kichwa cha Crónica kilikuwa: “Onyesho Jingine la Ajabu la Imani katika River na Vélez—Mashahidi Wabatizwa.” Hudhurio katika mikusanyiko yote miwili lilifanya jumla ya zaidi ya 67,000.
Upendezi wa Kimataifa
Mtu alipopita miongoni mwa wahudhuriaji waliovalia kwa rangi za kutokeza, tofauti za kimwili za rangi na tamaduni zilionekana wazi. Hapa palikuwa na dada Mwargentina aliyekuwa akifurahia yerba maté, chai iliyonywewa kupitia bombila ya chuma, au mrija, kutoka katika kikombe cha pekee cha mbao. Miongoni mwa Wahispania 800 walikuwamo akina dada waliovalia mavazi yenye kupendeza ya nchi hiyo. Kile kikundi cha watu 900 kutoka Japani kilikuwa ni kutia na wanawake wengine waliovalia kimono za kienyeji. Mjumbe kutoka Meksiko alivaa suti nyeusi na kofia ya sombrero ya Kimeksiko yenye uviringo mpana. Hata hivyo, licha ya tofauti zote hizi, umoja wao wa kiroho ulionekana wazi kwa wote. Mwishoni mwa kusanyiko wengi walibadilishana hiba—beji za mkusanyiko, kalamu, kadi za kutuma—chochote kile ambacho kingekumbusha tukio hili lenye kupendeza.
Roho ya kusanyiko ilifurika hadi kwenye nyanda za ndege. Hili lilikuwa dhahiri hasa katika Miami, Florida, U. S. A., ambapo vikundi vingi vilikutana wakitaka kusafiri. Wakirudi kutoka Buenos Aires, kikundi kikubwa kutoka United States kilikutana na kikundi cha Japani, ambao walikuwa wanaelekea Meksiko. Upesi, wasafiri Waamerika wakifungwa sana na maneno mengi ya wenzao Wajapani. Watu katika mahali pale walishindwa na wakavutiwa na lililokuwa likiendelea. Walikuwa Mashahidi wakionyesha roho yao ya “lugha iliyo safi”!
Programu ya mkusanyiko na ushirika wa kimataifa ulikuwa wenye kuchochea sana hivi kwamba mkusanyiko ulipomalizika Jumapili, hakuna mtu aliyependa kuondoka kwenye stediamu. Vikundi vya mataifa mbalimbali vilianza kuimba nyimbo za Ufalme katika lugha zao bila chombo chochote cha muziki, na wakapungiana vitambaa. Hili liliendelea kwa muda wa saa moja kabla ya wakusanyikaji wenye furaha kwenda nyumbani. Kama vile mpigaji picha mmoja wa siku nyingi Mwargentina alivyosema: “Hili halijawahi kutukia katika Argentina . . . hisia ya ndani kama hiyo na uchangamfu!”
[Picha katika ukurasa wa 15]
Zaidi ya 67,000 walihudhuria ”Lugha Iliyo Safi” Mikusanyiko ya Mashahidi wa Yehova katika Buenos Aires, Desemba 6-9, 1990
[Picha katika ukurasa wa 16]
Jengo-tata lililojipya la tawi la Argentina liko tayari kutumikia Mashahidi zaidi ya 84,000