Kumsifu Yehova kwa Korasi Iliyounganika
‘KUIMBA kulikuwa jambo ambalo lilifanya misisimuko hadi kwenye uti wa mgongo na kukaleta machozi machoni—kulikuwa kutamu sana. Hakukuhitajiwa vyombo vya muziki, na kilichoonekana kuwa muziki wa sauti fulani ngumu kilifanywa kuwa rahisi ajabu. Upatano wa sauti hiyo ulikuwa mtamu sana.’
Hisi hii ya ndani ilionyeshwa na aliyekuwa msimamizi wa Watch Tower Society, Nathan H. Knorr, baada ya kuhudhuria mkusanyiko wa Mashahidi wa Yehova katika Zambia. Inaonyesha vizuri uvumi wenye kuchochea wa mamia ya sauti za Waafrika zilizoinuliwa kwa wimbo wa upatano wa sauti.
Kuimba ni sehemu ya utamaduni wa Kiafrika. Katika kijiji cha Afrika, si ajabu kuona wanawake wakiimba namna ya nyimbo za kitamaduni wanapolima, vijana wakivuma nyimbo zao wanazopenda sana wanapokamua ng’ombe, na wanaume wakiimba nyimbo zenye kurudiwa-rudiwa kana kwamba kuwatia moyo ndume wao wavurute mizigo yao mizito. Kuna wimbo wa kila kazi kijijini.
Katika shule nyingi za Afrika, watoto hufunzwa kuimba kwa njia ya mfumo wa silabi za muziki. Mfumo huo wa kuonyesha kiwango cha sauti ya muziki ni nini? Kwa msingi, ni ule utaratibu wa “do, re, mi” mfikio uliofanywa na sinema moja ya muziki yenye sifa miaka kadhaa iliyopita. Do, re, mi, fa, sol, la, ti, hulingana na zile sauti moja moja nane za muziki zinazopigwa kwa vyombo vya muziki vya nchi za Magharibi. Mfumo huu wa herufi za muziki hutumia nukta mbili, vistari, alama za vituo, na kanuni za kuonyesha hesabu ya mipigo katika kifungu na mwendeleo wa herufi za muziki. Sauti hizo nne (saprano, alto, tenor, na bass) zimepangwa moja chini ya nyingine, na ni mpatanisho huu wa sauti ambao hutoa muziki huo wenye kuchochea nafsi. Wengi hukubali kuwa njia hii ni rahisi sana kujifunza na kuimba kuliko kwa mfumo wa herufi za muziki.
Hivyo basi, nyimbo zilizo katika kitabu cha nyimbo kinachotumiwa na Mashahidi wa Yehova, Mwimbieni Yehova Sifa, zilinakiliwa kwa njia ya mfumo wa kuonyesha kiwango cha sauti ya muziki kwa nakala zote za Kiafrika. Kwanza, muda wa saa nyingi ulitumiwa kwenye piano ili kulinganisha nyimbo hizo na sehemu za sauti nne zenye ulinganifu. Kisha, kila ya sauti hizo ilibadilishwa katika mfumo wa herufi za muziki. Halafu, mtu mwenye kujua mfumo wa silabi za muziki alipewa mgawo wa kuimba kila sauti ya kila wimbo kuhakikisha usahihi wa kila herufi. Kompyuta zilitumiwa kupanga mfumo wa kutumia silabi za muziki kuonyesha kiwango cha sauti ya muziki pamoja na maneno ya kila wimbo. Mwishowe iliwezekana kuchapa muziki wenye kusomeka kwa urahisi unaoona kwenye ukurasa huu.
Matokeo? Mashahidi wa Yehova Afrika wanaweza kupatanisha sauti zao kwa sifa yenye shangwe kwa Yehova. Maneno ya wimbo wao mmoja huonyesha hisia zao vizuri: “Twapiga kelele kwa ushindi, twapiga makofi. Mengi Mungu ametufanyia sisi! Sauti zetu zafurikwa kwa sifa yenye shangwe kwa korasi yenye kuunganika.”
[Mchoro of kingdom song in sol-fa method katika ukurasa wa 30]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)