Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 11/8 kur. 28-29
  • Kuoana au Kuishi Pamoja—Jambo Jipi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuoana au Kuishi Pamoja—Jambo Jipi?
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuishi Pamoja—Je! Kuna Mafaa?
  • Ndoa—Njia Iliyo Bora
  • ‘Na Waoane’
  • Kuna Ubaya Gani Kuishi Pamoja Kabla ya Kuoana?
    Amkeni!—2009
  • Kutayarisha Kwa Ajili Ya Ndoa Yenye Mafanikio
    Siri ya Furaha ya Familia
  • Je, Tuishi Pamoja Kabla ya Ndoa?
    Msaada kwa Ajili ya Familia
  • Biblia Inasema Nini Kuhusu Ndoa?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 11/8 kur. 28-29

Maoni ya Biblia

Kuoana au Kuishi Pamoja—Jambo Jipi?

“NI LINI tutafunga ndoa?” Miaka 35 tu iliyopita, huenda wenzi wawili waliopendana walitafakari swali hilo walipokuwa wakichumbiana. Leo hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa kwamba swali hilo lingetokezwa na watu wawili ambao tayari wamekuwa wakiishi pamoja. Nyakati zimebadilika na ndivyo na mielekeo kuhusu ndoa. Ni njia ipi iliyo bora: Kufunga ndoa au kuishi tu na mtu uliyechagua?

Uchunguzi unaonyesha kuwa katika Brazili, Ufaransa, Sweden, United States, na nchi nyinginezo nyingi, kuishi pamoja bila kufunga ndoa ndio mtindo. Huenda ikapatana na desturi ya kisasa, lakini si jambo jipya. Lililo jipya ni mitazamo kuelekea tendo hilo. Lililokuwa likionekana kuwa ni kuishi kwa dhambi hapo zamani ndilo sasa linaachiliwa au kukubaliwa na wengi kuwa sawa kabisa.

Kuishi Pamoja—Je! Kuna Mafaa?

Watu wengine hutoa hoja kwamba mpango wa njoo-tukae ni wa maana, kwa kuwa huwezesha wenzi wawili kujuana vizuri kabla ya kuingia katika kifungo cha daima. Mafaa mengine ambayo watu fulani hutoa ni haya: Huwezesha wenzi wawili wapunguze gharama kwa kushirikiana kulipa kodi; huwapa uhuru wa kutotegemea wazazi; huandaa urafiki unaohitajiwa, kutia ndani uhusiano wa ngono. Wenzi wa umri mkubwa wasiofunga ndoa husema kwamba kwa kuishi pamoja hawapotezi malipo ya usalama ya serikali.

Hata hivyo, hoja moja kubwa dhidi ya kuishi bila kufunga ndoa ni hii: Mmoja au mwingine anaweza kuvunja mpango huo wakati wowote kwa kwenda tu. Kwa kweli gazeti la kila siku la Ufaransa Le Monde liliripoti kwamba katika Sweden na Norwei, nusu ya uhusiano wa njoo-tukae haumalizi miaka miwili, na kuanzia asilimia 60 hadi asilimia 80 huvunjika katika muda usiozidi miaka mitano.

Ndoa—Njia Iliyo Bora

Wale ambao hutetea mpango wa njoo-tukae huenda wakakiona cheti cha ndoa kuwa “karatasi” tu, kitu ambacho hakina thamani yoyote. Mwelekeo huu pia unaonyeshwa na mfululizo wa vipindi vya michezo ya kuigiza katika TV na sinema, pia katika maisha ya faragha ya watu maarufu. Kwa hiyo, hebu tuchunguze sasa thamani ya kweli ya “karatasi” hiyo.

Unapoingia ushirika wa biashara au kununua mali au kumkopesha mtu pesa, kwa nini huwa unaandika mapatano na hata kuhakikishwa na wakili? Sababu moja ni kwamba wote wawili wamejifunga wajibu, na ni kwa mafaa ya wote kuandika mapatano. Mathalani, mtu mmoja akifa, atoroke, au hata apoteze kumbukumbu lake, mapatano hayo bado yanatumika kihalali. Ndivyo ilivyo na ndoa. Katika tukio la kifo cha mwenzi mmoja wa ndoa au wote wawili, mamlaka katika nchi nyingi hutoa uandalizi kwa washirika waliobaki wa familia. Jambo hilo hukosekana katika mpango wa njoo-tukae. Ni wajibu huu unaotofautisha kati ya kuishi pamoja, na kufunga ndoa. Na cheti cha ndoa ni kikumbusha cha wajibu huo kwa wenzi wa ndoa kupendana, kuheshimiana, na kutunzana na cha maana za nadhiri za ndoa kulingana na sheria.

Mwanamke mmoja aliyeolewa alisema hivi: “Labda mimi ni mshamba lakini sharti ya ndoa hunifanya nihisi mwenye usalama sana.” Yeye hurudia kusema yale ambayo Mungu alisema alipofunganisha ndoa wale wanadamu wawili wa kwanza: “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”a (Mwanzo 2:24) Umoja usio na kifani! Hivyo, inawezekana kuwa na “mwili mmoja” katika uhusiano ulio kamili, bila kutia mwingine, halali, na wa muda wote—si penginepo pote.

Hata hivyo, watu wengine hutoa hoja kwamba wanajua wenzi wanaoishi pamoja bila kufunga ndoa na bado wana uhusiano mzuri sana.

‘Na Waoane’

Biblia hutoa sababu nzuri kwa wenzi kutokaa pamoja bila kufunga ndoa. “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu,” yasema Waebrania 13:4. Biblia husema waziwazi kwamba kuishi pamoja nje ya kifungo cha ndoa ni uasherati. Ni nini basi linalomaanishwa na “uasherati”? Kamusi moja huufafanua kuwa “uhusiano wa ngono wa kibinadamu isipokuwa kati ya mume na mke wake.” Ili tuwe na dhamiri safi, ni lazima tufuate shauri hili la Biblia: ‘Mapenzi ya Mungu ni kwamba mwepukane na uasherati.’—1 Wathesalonike 4:3.

Lakini iweje mtu akiwa na tatizo la kuzuia tamaa zake za ngono? Mtume Paulo aliandika: “Ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.” Na tena: “Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, . . . na awaruhusu waoane.” (1 Wakorintho 7:9, 36) Ona kwamba Paulo hakusema ‘wafanye watakavyo na kuishi pamoja’ bali, ‘Na waoane.’

Si kwamba ndoa inapasa kuonwa kuwa njia ya kutosheleza tamaa za ngono. Wenzi wawili wanapaswa kujuana vizuri kabla ya kuoana. Lakini waweza kufanyaje hivyo isipokuwa mwishi pamoja? Uchumba wenye kuheshimika hutoa fursa ya kutosha kwa jambo hilo. Unapaswa kutambua lile unalotazamia kwa ndoa yako na mwenzi wako wa ndoa. Mahitaji yako ya kimwili, kihisia-moyo, na ya kiroho ni nini? Je! mtu unayemfikiria kuwa aweza kuwa mwenzi wako atakusaidia uyatimize?—Mathayo 5:3.

Baada ya kuchunguza yaliyo juu, bila shaka utakubali kuwa njia hizo mbili—kuishi pamoja au kufunga ndoa—la mwisho ndilo bora. Wenzi wanaoishi pamoja katika ndoa hufanya hivyo bila lawama au woga, na wanafurahia heshima kutoka kwa marafiki na watu wa ukoo. Watoto wao hawatakuwa na makovu ya kihisia-moyo kwa sababu ya kuzaliwa nje ya kifungo cha ndoa. Na jambo la maana zaidi, wenzi hao humpendeza Mungu kwa kuonyesha heshima kwa mpango wake wa ndoa.

[Maelezo ya Chini]

a Neno la Kiebrania da·vaqʹ (“ambatana”) “huwa na maana ile ile na kushikamana na mtu kwa upendo na ushikamanifu.” (Theological Wordbook of the Old Testament) Katika Kigiriki, ni asili ile ile ya neno linalomaanisha “kuambatishwa kwa gundi,” “kupiga sementi,” “kuunganisha pamoja kikiki.”

[Picha katika ukurasa wa 28]

Arusi ya karne ya 16

[Hisani]

Picha ya Pieter Bruegel mkubwa, yenye kuonyesha Arusi ya Washamba, karne 16, imetolewa kwa idhini ya Kunsthistorisches Museum, Vienna

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki