Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 11/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Jilinde na Muziki Usiofaa!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Muziki Wangu Una Ubaya Gani?
    Amkeni!—1993
  • Muziki Waweza Kweli Kuniumiza?
    Amkeni!—1993
  • Je, Utafanya Maamuzi Yenye Hekima?
    Amkeni!—2011
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 11/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Sayansi Naandika kuwapongeza kwa ajili ya mfululizo wenu wa sehemu sita “Sayansi—Jitihada Inayoendelea ya Ainabinadamu ya Kutafuta Kweli.” (Aprili 8 hadi Juni 22, 1993) Makala zenu hazikupendelea na zilikuwa zenye kuarifu. Nikiwa mwanasayansi, nilishangaa kujifunza jinsi wanafalsafa Wagiriki, yaani Aristoto, Plato, na wengine, wamekuwa na uvutano juu ya dhana ya sayansi.

O. O., United States

Katika sehemu ya sita ya mfululizo wenu (Juni 22, 1993), mlisema: “Ule uharibifu wa mazingira ambao sayansi imesababisha ni mkubwa sana.” Sayansi si ya kulaumiwa kwa ajili ya utumizi mbaya wa ubuni wayo. Serikali zinazotumia njia zisizofaa za kisheria ili kusimamia utumizi wa teknolojia ndizo za kulaumiwa.

C. C. R., United States

Mfululizo huo haukujaribu kuwalaumu wanasayansi pekee kwa ajili ya matatizo ya kimazingira ya dunia. Kwa kweli, sentensi iliyotangulia ilisema waziwazi kwamba sayansi “imechangia kuleta” matatizo hayo. Makala zilizotangulia katika mfululuzo huo zilionyesha kwamba ni lazima wanasayansi washiriki lawama na wanasiasa, wanabiashara, na wateja.—Mhariri.

Kuwa Pekee Asanteni kwa simulizi la maisha ya Pepita Abernathy, “Maisha Yenye Kuthawabisha Nijapokuwa Pekee.” (Februari 22, 1993) Ilileta machozi machoni pangu. Sikuzote nimepata ikiwa vigumu kuhubiri marafiki au kufanya kazi kwenye eneo lisilo na matokeo mazuri. Lakini Pepita Abernathy alihubiri katika sehemu mbalimbali za ulimwengu hata wakati ambapo hakujua lugha yenyewe! Sasa nina mtazamo tofauti kuelekea kazi ya kuhubiri.

J. W., United States

Muziki Nimetoka tu kumaliza kusoma mfululizo “Muziki wa Kisasa—Raha Isiyodhuru?” (Juni 8, 1993) Nilipokuwa katika shule ya sekondari, nilisisimuliwa na muziki wa mdundo mzito. Mazoea yangu mabaya na mtazamo wa uasi ulikuwa tokeo la mawazo yaliyotokezwa na muziki huo wenye uovu na giza. Lakini kadiri nimemkaribia Yehova zaidi, ndivyo nimekuja kuchukia hata sauti ya muziki huo!

L. K., United States

Mmetupa sisi vijana shauri lenye kutumika linalotegemea vyanzo vya kisiku-hizi vinavyotegemeka. Watu fulani wamefikiri kwamba muziki wakubalika maadamu huwezi kuonwa kuwa wa mdundo mzito au rapu, hata ukitia moyo ukosefu wa adili, jeuri, na utumizi wa madawa. Makala hizo zimekatalia mbali wazo hilo lisilofaa. Sasa sisi sote twajua jinsi ya kuwa wateuzi zaidi tunapochagua muziki.

F. M., Italia

Mwanangu tineja alitengwa hivi karibuni kutoka kwa kutaniko la Kikristo. Nilijaribu kadiri niwezavyo kumfanya aache kusikiliza muziki wa rapu—nikisababu naye, nikimwonyesha kanuni za Biblia, nikishiriki makala naye juu ya jambo hilo. Lakini yeye aliendelea kusikiliza rapu kwa siri, akihisi kwamba haukuwa na athari yoyote kwake. Hata hivyo, yeye alikuja kufanya yaliyo mengi kati ya mambo mabaya yanayotukuzwa katika muziki huu. Bado mimi sijatulia kihisiamoyo kutokana na kuanguka kwa mwanangu. Ni tumaini langu kwamba wazazi wote Wakristo wataonyesha uthamini kwa habari hii kwa kuisoma na kujifunza pamoja na watoto wao.

G. C., United States

Hamwonyeshi tu ni aina gani ya muziki inayopaswa kuepukwa, bali pia mwategemeza maneno yenu kwa kutoa sababu zisizokanushika, na bado zenye upole na upendo. Twahisi kwamba tamaa yenu kuu ni kusaidia vijana wautoroke ulimwengu huu wenye ufisadi mkubwa.

B. V., Ufaransa

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki