Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 2/8 kur. 15-17
  • Muziki Wangu Una Ubaya Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Muziki Wangu Una Ubaya Gani?
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Muziki—Mahali Pao Maishani
  • Ule Uvutano wa Muziki wa Roki
  • Ujumbe wa Rapu
  • Mtindo wa Maisha wa Rapu
  • Jilinde na Muziki Usiofaa!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Muziki Waweza Kweli Kuniumiza?
    Amkeni!—1993
  • Raha Isiyodhuru au Sumu ya Akili?
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 2/8 kur. 15-17

Vijana Wanauliza . . .

Muziki Wangu Una Ubaya Gani?

“Babangu husema, ‘Komesha kelele hiyo! Inaumiza masikio yangu!’”—Mvulana tineja.

“Baadhi ya muziki wa rapu ni wenye kuchukiza sana, sana. —Msichana tineja.

“SI JAMBO la maana sana,” akalalamika Jodie. “Kwa nini wanafanya muziki wangu kuwa suala kubwa?” Lisette wa miaka kumi na mitatu ahisi vivyo hivyo. “Ni wimbo tu,” asisitiza.

Je! wewe vilevile umo katika mzozano wenye kuendelea na wazazi wako juu ya muziki? Ikiwa ndivyo, huenda ukakabiliwa na malalamishi, vitisho, na amri kila wakati unapowasha kaseti au rekodi yako uipendayo zaidi. (Babangu husema, ‘Komesha kelele hiyo! Inaumiza masikio yangu!’” asema mvulana mmoja tineja. Kwa kuchoshwa na ugomvi huo, huenda ukahisi kwamba wazazi wako wanafanya suala kubwa kutokana na jambo dogo. “Namna gani wakati wao walipokuwa wachanga?” abisha msichana mmoja tineja. “Je! wazazi wao hawakufikiri muziki wao ulikuwa mbaya?”

Msichana huyo ana jambo lipasalo kufikiriwa. Muda wote wa historia, vizazi vya umri mkubwa na vya umri mchanga vimeelekea kupambana juu ya mambo ya upendezi wa kibinafsi. Kwa hiyo kwa nini uache kusikiliza muziki wako kwa sababu tu wazazi wako hawaupendi? Isitoshe muziki wako una ubaya gani?

Muziki—Mahali Pao Maishani

Naam, kwa kweli hakuna asemaye kwamba ni kosa kufurahia muziki. Sehemu fulani za Biblia yenyewe—hasa zaburi—mwanzoni zingeweza kuimbwa. Katika nyakati za Biblia, muziki ulitumiwa sana katika ibada ya Mungu. (Zaburi 149:3; 150:4) Muziki pia ulitumika kuwa njia ya kuonyesha shangwe, msisimuko, na huzuni. (Mwanzo 31:27; Waamuzi 11:34; 1 Samweli 18:6, 7; Mathayo 9:23, 24) Katika siku za Yesu Kristo, muziki ulikuwa sehemu ya kawaida katika vikusanyiko vya kijamii; uliongeza kuonea shangwe pindi hiyo.—Luka 15:25.

Muziki huendelea kuwa na fungu la maana leo—hasa miongoni mwa vijana. The Journal of the American Medical Association lasema hivi: “Kati ya umri wa miaka 12 na 18, tineja wa wastani husikiliza muziki wa roki kwa saa 10,500, huo ukiwa muda ulio chini kidogo tu ya jumla ya saa atumiazo darasani tokea nasari hadi sekondari.”

Uchunguzi huonyesha kwamba idadi kubwa zaidi ya vijana wa U.S. husikiliza karibu muziki wa roki na popu pekee. (Ili kurahisisha mambo, tutatumia maneno “roki” na “popu” kutaja karibu mitindo yote ya muziki upendwao zaidi na vijana—tokea muziki wa soli na wimbi mpya hadi rapu na mdundo mzito.) Kulingana na The World Book Encyclopedia, “muziki wa roki si muziki wa vijana Waamerika tu tena. Ni muziki wa ulimwengu.”

Ule Uvutano wa Muziki wa Roki

Kwa nini muziki wa roki unapendwa sana hivyo? Kulingana na kitabu Youth Trends, roki hutumika kuwa “lugha inayoshirikiwa na vijana wote.” Hivyo baadhi ya vijana huhisi kwamba kujua ni muziki gani unaopendwa zaidi katika ulimwengu wa muziki—kujua vile vikundi vipya na nyimbo mpya zaidi—huwasaidia kukubalika na vijana wengine. Muziki huandaa kifungo cha umoja miongoni mwa vijana na mambo yasiyo na mwisho ya kuzungumzia.

Hata hivyo, kwa wengine, muziki hufurahiwa zaidi wakiwa peke yao. Je! umekuwa na siku ngumu shuleni? Basi labda wewe ni kama yule msichana tineja aitwaye Bree asemaye: “Mimi huketi chumbani mwangu, naweka stereo sauti kubwa kwelikweli na kuketi humo tu. Ni kama unaniondolea mkazo na msongo.” Ingawa muziki wa roki mara nyingi huchambuliwa kuwa wenye kelele na kuumiza masikio, nyimbo nyingi zipendwazo sana zina melodia zenye kupendeza na sauti tamu za muziki wa okestra.

Ingawa hivyo, kwa wengi, liwavutialo ni mdundo. “Ndio muziki ulio rahisi zaidi wa kucheza dansi,” akaeleza msichana mmoja alipoulizwa kwa nini yeye ni shabiki wa muziki wa rapu. Lakini wengi pia wanavutiwa na maneno. Yakiandikwa hasa kwa ajili ya vijana, maneno ya popu huwa na unamna-namna mwingi wa hisia na mahangaiko ya vijana. Muziki wa rapu unajulikana hasa kwa kukazia masuala ya wakati wa sasa, kama vile ubaguzi wa rangi na utovu wa haki za kijamii. “Mimi hufungua redio na muziki ulio mwingi zaidi haueleweki, hunitia kichaa,” alalamika tineja mmoja jina lake Dan aliyenukuliwa katika gazeti Newsweek. “Rapu una hadithi halisi na vitu halisi. Unapendeza kuusikiliza.”

Hata hivyo, ujumbe ndio uwahangaishao zaidi wazazi wako.

Ujumbe wa Rapu

Kwa mfano, fikiria muziki wa rapu. Katika muziki wa rapu, yale maneno—maneno yasiyo ya ufasaha yatumiwayo barabarani za miji ndiyo yatumiwayo—hunenwa, si kuimbwa, yakifuatanishwa na mdundo wenye nguvu. Bila shaka, hakuna lililo ovu kiasili katika wazo hilo. Nyimbo nyingi zipendwazo sana kwa muda wa miongo iliyopita zilishirikisha maneno ya kutamkwa. Lakini muziki wa rapu mara nyingi huchukua wazo hilo kwenye hatua yenye kupita kiasi sana.

Rapu (au, hipu-hopu) ulipata kuwa wenye kupendwa na wengi sana huko nyuma katika miaka ya 1970 katika vilabu vidogo vya kuchezea dansi Jijini New York ambamo vijana wa mjini walizoea kwenda. Wapiga rekodi walipoanza kuimba-imba maneno au kuyatamka kimashairi kwa kufuatana na midundo iliyotangulia kurekodiwa, wacheza dansi waliitikia karibu kwa kichaa. Upesi muziki wa rapu ukatoka barabarani na vilabuni vya chini ya ardhi na kuingia katika mifumo mikuu ya kimuziki. Majina ya wanamuziki wa rapu yenye ufidhuli kama muziki wao—Adui ya Umma, M.C. Hammer, na “Vanilla Ice”—upesi yakawa yakijaza mawimbi ya hewani na aina yao ya muziki.

Kwa kupendeza, ripota wa Amkeni! alipouliza kikundi cha vijana Wakristo wa kiungani chenye mchanganyiko wa rangi, “Je! wengi wenu husikiliza rapu?” idadi kubwa zaidi kushangaza ilisema ndiyo! Kisha akauliza, “Ni jambo gani mnalopenda kuhusu rapu?” “Ule mdundo,” akajibu msichana mmoja tineja. “Unatiririka tu, na ni rahisi kuusikiliza.” “Unaweza kucheza dansi kuufuata,” akajibu mwingine. Hata hivyo, swali lililofuata halikutokeza jibu lenye idili kadiri hiyohiyo, “Je! baadhi ya muziki wa rapu ni tatizo kwa Wakristo?”

Baada ya kimya chenye kutia haya, msichana mmoja akakubali hivi: “Baadhi ya muziki wa rapu ni wenye kuchukiza sana, sana.” Wengine wakaafikiana naye shingo upande. Kwelikweli, iligunduliwa kuwa wengi kati ya vijana walifahamiana kwa njia yenye kushtua na orodha ndefu ya nyimbo zenye kuchukiza—nyimbo zilizotia moyo uasherati na upotovu kwa maneno yaliyo waziwazi sana. Baadhi yao walikiri kwamba nyingi za nyimbo hizo zilitumia sana matusi.

Ndiyo, muziki mwingi wa rapu huonekana ukipeleka ujumbe wa uasi, jeuri, ubaguzi wa rangi, na uhodari wa kufanya ngono. Mwendelezaji wa rapu Daniel Caudeiron, msimamizi wa “Black Music Association of Canada,” asifuye rapu kuwa “unafaa sana,” alikubali kwamba muziki mwingi wa rapu “hushambulia wanawake, ni wenye kutia moyo ngono na pindi kwa pindi ni wenye kutumia matusi.”—Maclean’s, Novemba 12, 1990.

Mtindo wa Maisha wa Rapu

Inakubalika, muziki wote wa rapu si wenye ukosefu wa adili au wenye jeuri. Kulingana na makala moja katika The New York Times, baadhi yao hujitoa kuendeleza miradi ifaayo kama vile elimu, kuvunja moyo matumizi ya dawa za kulevya, na kutatua maovu ya kijamii. Lakini maneno yasiyochukiza yaweza sana kuwa siyo kawaida. Wakati Newsweek lilipokadiria rekodi kumi zenye kupendwa zaidi, likitumia kiwango kama kile kitumiwacho na ule mfumo wa kukadiria sinema za U.S., ni mbili tu zilizofikiriwa kuwa G, au ziwafaazo wasikilizaji kwa ujumla. Newsweek lilikadiria nne kati ya rekodi hizo kuwa R (zinazoruhusiwa watu wazima pekee), na mbili hata zilikadiriwa kuwa X kwa sababu ya “lugha chafu” na ngono zenye kuonyeshwa waziwazi sana.

Zaidi ya hilo, ujumbe wa muziki wa rapu huenda mbali kupita maneno yao. Muziki wa rapu umetokeza mapinduzi ya kitamaduni. Mamilioni ya matineja huvaa mavazi makubwa mno, viatu vifikavyo juu ya vifundo vya miguu na vyenye kamba zilizoachwa bila kufungwa, jins kubwa-kubwa, mikufu ya dhahabu, kofia za besiboli, na miwani myeusi ambayo ndiyo mavazi rasmi ya vikundi vya rapu. Wengi huiga pia ishara za mwili na mitazamo yenye majivuno kupita kiasi ya wachezaji wa muziki wa rapu. Na kwa fadhaa ya wazazi na walimu, maneno yasiyotumiwa kwa kawaida kama vile “yo!” na “dis”—maneno yasiyo ya ufasaha yenye kuudhi yatumiwayo na vijana wa mjini yatukuzwayo katika muziki wa rapu—yameingizwa katika uneni wa kila siku.

Huenda muziki wa rapu ukawakilisha uasi dhidi ya utovu wa haki. Lakini ukionwa kwa ujumla, muziki wa rapu pia ni utamaduni wa uasi dhidi ya viwango vya kimungu vya mwenendo, mavazi, na uneni. Je! kwa muziki aupendao, Mkristo ataka kuhatirisha kuvutwa kwenye mtindo kama huo usiyofaa wa maisha?

Bila shaka, muziki wa rapu sio tu namna ya muziki upitao kiasi. Gazeti Times huripoti hivi: “Kuna ladha chungu katika karibu kila eneo la utamaduni wa Amerika wa ki-siku-hizi upendwao zaidi. Mabingwa wa muziki wenye mdundo mzito Motley Crue huabudu sanamu za ushetani na kikundi cha “Beastie Boys” huigiza kupiga punyeto jukwaani.” Biblia ilitabiri kwamba katika “siku za mwisho . . . watu wabaya na wadanganyaji [wangeendelea], na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.” (2 Timotheo 3:1, 13) Basi, je! ikushangaze kwamba muziki mwingi wa leo hupelekea vijana Wakristo ujumbe mbaya?

Kwa hiyo huenda wazazi wako wakahangaika kwa kufaa ikiwa wewe huvutiwa na rapu au namna nyingineyo ya muziki wa roki wenye kupita kiasi. Huenda wakahofu kwamba kusikiliza daima muziki kama huo kutakudhuru. Je! hofu zao zaweza kuwa halali? Toleo letu lijalo litazungumzia swali hilo.

[Picha katika ukurasa wa 17]

Vijana wengi sasa huiga mavazi na mitazamo ya wachezaji wa muziki wa rapu

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki