Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 2/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wazoefu wa Kamari Wafaransa
  • Waswedeni Wachache Huenda Kanisani
  • Vikumbusho Hatari vya Vita ya Ulimwengu 2
  • Hakuna Fedha za Kuokoa Uhai
  • Matumizi Mengineyo ya Divai Wakati wa Misa
  • Hatari Mpya ya Kipindupindu
  • Japani Yataka Wenye Kuacha Uvutaji
  • Jeuri ya Mahali pa Kazi
  • Yen Yenye Kupanda Sana Thamani
  • Vyakula vya Kosha ni Afadhali?
  • Watu wa Australia Wanaozeeka
  • Kuna Ubaya Gani Kucheza Kamari?
    Amkeni!—2002
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1992
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1995
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 2/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Wazoefu wa Kamari Wafaransa

Ujapokuwa ukosefu unaoongezeka wa kazi ya kuajiriwa na hali ya kiuchumi ya Ulaya inayozidi kuwa mbaya, Wafaransa wanatumia fedha nyingi zaidi ya wakati mwingine wowote katika kucheza kamari na kubahatisha, yasema INSEE (Taasisi ya Kitaifa ya Uchunguzi wa Tarakimu ya Ufaransa). Franks zaidi ya bilioni 70 zilichezwa kamari katika 1992, asilimia 16 zaidi ya mwaka uliopita. Kwa wengi, tamaa ya kucheza kamari imekuwa isiyoongozeka. “Ni uzoefu usio wa madawa,” asema mtaalamu wa akili Jean Ades aliye Mfaransa. “Kukiwa na hesabu inayoongezeka ya njia za kubahatisha . . . na wimbi kubwa daima la ujumbe kutoka kwa matangazo na vyombo vya habari unaowatia watu moyo wabahatishe, watu wengi zaidi na zaidi wanagundua kwamba wao ni wazoefu.” Wacheza kamari ni wazoefu “wanapoanza kubahatisha fedha zilizo zaidi ya zile walizo nazo na kupuuza matokeo ya kifedha yatakayowapata wao na familia yao kwa ajili ya tabia yao,” laripoti gazeti la Ufaransa Le Monde, na “kucheza kamari ni mojapo aina za uzoefu zilizo ngumu zaidi kutibu.” Mtu mmoja aliyekuwa mzoefu wa madawa ya kulevya asema: “Ilikuwa rahisi kuacha kutumia madawa ya kulevya kuliko kuacha kucheza kamari.”

Waswedeni Wachache Huenda Kanisani

Uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Maoni ya Umma ya Swedeni kwa niaba ya Kanisa la Swedeni waonyesha kwamba kati ya wale watu zaidi ya 1,000 walioulizwa kama wanaamini kuna Mungu, asilimia 47 walijibu ndiyo. Hata hivyo hudhurio la Kanisa halionyeshi hivyo. Kati ya wale waliohojiwa, ni asilimia 9 tu wanaoenda Kanisani kwa kawaida. “Watu hawaendi Kanisani hadi wanapohisi tazamio kwamba ni huko ndiko wanakoweza kupata kile wanachotafuta,” asema Anders Swärd, naibu mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kanisa la Swedeni.

Vikumbusho Hatari vya Vita ya Ulimwengu 2

Karibu miaka 50 baada ya mwisho wa Vita ya Ulimwengu 2, jiji la Ujerumani la Hamburg bado lina vikumbusho hatari vya vita hiyo. Gazeti Süddeutsche Zeitung laripoti kwamba katika kipindi cha miezi 12 kilichoisha katika Julai 1993, washiriki 23 wa Kikosi cha Kuharibu Silaha cha jiji kiliharibu mabomu zaidi ya 500, makombora 2,440, gruneti za mkono 97, vitupa-roketi 24 vya kulipua vifaru, baruti 4 za kulipua vifaru, na kilo 149 za baruti nyinginezo zilizo ardhini na majini katika Hamburg. Kulingana na makadirio, kuna mabomu 2,000 mengineyo katika ardhi ya jiji hilo. “Itachukua vizazi vingine viwili kuweza kuyaondolea mbali,” likaripoti gazeti hilo.

Hakuna Fedha za Kuokoa Uhai

Ingawa maradhi ya mchochota wa pafu na kuhara yaweza kutibika, hayo huua watoto wapatao milioni 7.5 kila mwaka, yaripoti idara ya habari ya Agence France-Presse. Ulimwenguni kote, watoto walio chini ya umri wa miaka mitano huathiriwa na visa vipatavyo milioni 40 vya mchochota wa pafu na zaidi ya visa bilioni moja vya kuhara. Hata hivyo, Daktari Ralph Henderson wa WHO (Shirika la Afya Ulimwenguni) alikiri kwamba magonjwa hayo ni “rahisi na si ghali kutibiwa.” Kwa kusikitisha, ilibidi programu nyingi zinazopangwa na WHO ili kupigana dhidi ya magonjwa hayo mawili ziachwe au ziahirishwe kwa wakati usiojulikana kwa sababu ya shida za kifedha. Kulingana na WHO, nusu ya vifo vinavyotokana na kuhara na theluthi moja ya vile vinavyosababishwa na mchochota wa pafu vyaweza kuepukwa ikiwa fedha zingepatikana.

Matumizi Mengineyo ya Divai Wakati wa Misa

Ugunduzi wa hivi karibuni waonyesha kwamba ingawa lita 10,000,000 za divai huuzwa kila mwaka ili zitumiwe kwenye Misa katika Italia, “unywaji mtakatifu” hutumia lita 1,000,000 pekee. Kwa nini kuwe na tofauti hiyo? Kulingana na mstadi mmoja, “ile desturi ya kisiri ya watoto wa misa na msakiristi kukonga [divai] haiwezi kutumia divai nyingi hivyo.” “Ukweli ni kwamba,” lasema Corriere della Sera, “unywaji huo huzidishwa mara kumi zaidi kwenye meza za mlo za maaskofu, makasisi na mapadri.”

Hatari Mpya ya Kipindupindu

Aina mpya ya kipindupindu ambayo imeenea upesi katika India na Bangladesh hadi Thailand huenda ikasababisha mweneo wa nane wa tufeni pote wa maradhi hayo tangu 1817, maofisa wa afya wasema. Maonyo yametolewa kwa nchi katika Asia, Afrika, na Amerika ya Latini. Mashambulizi ya mapema ya ugonjwa ule wa zamani zaidi hayatoi kinga ya kudumu dhidi ya huu mpya. Isitoshe, aina hii mpya haiwezi kugunduliwa kwa njia za kawaida za majaribio katika lebu, na madawa ya sasa hayana nguvu dhidi yayo. “Kwa kuwa hatuwezi kutabiri ni wapi au ni kwa kadiri gani kiini hicho kipya kitaenea, ni lazima nchi ziwe tayari wakati wote kwa kuendelea kufanya uchunguzi, kwa kuhakikisha mtu apata matibabu na kwa kuandaa maji safi na vyoo vifaavyo,” wakaandika madaktari David L. Swerdlow na Allen A. Ries wa Vitovu wa Udhibiti wa Maradhi, kama ilivyoripotiwa katika gazeti The Lancet. Mweneo wa saba, ulioanza katika Asia katika 1960, bado waendelea, kukiwa na visa zaidi ya milioni tatu na mamia ya maelfu ya vifo.

Japani Yataka Wenye Kuacha Uvutaji

Kulingana na Mainichi Daily News, Japani ina wavutaji sigareti wengi zaidi ya taifa jinginelo lililoendelea, kukiwa na asilimia 60 ya wanaume wazima wanaovuta sigareti. Ikitumaini kwamba wengi wataacha kuvuta, Wizara ya Afya na Hali-Njema ilitoa taarifa yenye onyo kwamba kuvuta sigareti huharibu uwezo wa kusikia, huharakisha kuzeeka, na husababisha ugonjwa wa akili, kudhoofika kwa mifupa, na kuzaliwa kwa vitoto vidogo zaidi. Ilisema kwamba sigareti zenye kiasi kidogo cha tumbaku hazifai katika kuepuka kusongwa kwa mishipa ya moyo. Wenye kuacha uvutaji huongeza uzito kwa karibu kilo mbili, lakini hilo halileti tatizo la afya. Ripoti hiyo ilipata kwamba ingawa asilimia 80 ya wavutaji sigareti hujaribu kuacha tabia hiyo, kupunguza hesabu ya sigareti zinazovutwa kila siku ni kama hakufanikiwi. Wizara hiyo ilisema kwamba njia bora zaidi ya kuacha uvutaji ni kuondolea mbali sigareti kabisa, na viwango vya mafanikio vyaweza kuwa maradufu wakati programu zilizoongozwa na madaktari zinapotumiwa.

Jeuri ya Mahali pa Kazi

“Wauguzi na wafanyakazi wengine wa afya hukabili jeuri kazini, mara nyingi karibu kama maofisa wa polisi,” laripoti The Vancouver Sun. Profesa wa mambo ya uhalifu Neil Boyd wa Chuo Kikuu cha Simon Fraser alifanya uchunguzi huo juu ya jeuri ya mahali pa kazi katika British Columbia, Kanada. Alipata kiwango cha hatari kwa maofisa wa polisi na wafanyakazi wa afya kuwa “mara nne zaidi ya kiwango cha kazi nyingineyo” na kwamba visa vya jeuri vimeongezeka kwa asilimia 400 tangu 1982. Wagonjwa ndio “karibu sikuzote walifanya jeuri dhidi ya wafanyakazi wa afya,” gazeti hilo likasema, na vitendo hivyo vilitokea mara nyingi zaidi wakati wa “kuamsha au kuosha mgonjwa.” Pia, uchunguzi huo ulionyesha kwamba “wafanyakazi wa makao ya kurekebisha-tabia, maofisa wa usalama wa kibinafsi, madereva wa teksi na mabasi na makarani wa maduka ya rejareja” hukabili hatari kubwa ya kupatwa na jeuri ya mahali pa kazi.

Yen Yenye Kupanda Sana Thamani

“Katika miaka 22 iliyopita, yen [ya Japani] imepatwa na mabadiliko yasiyo ya kawaida,” lasema The Wall Street Journal. “Haijapanda tu thamani kwa asilimia 225 dhidi ya dola katika kipindi hicho, bali pia imepewa sifa ipewayo fedha chache nyinginezo ulimwenguni. . . . Ili kupata maana ya badiliko hilo, nenda tu kwenye duka la mazulia katika Istanbul, ajiri mtembeza-wageni katika Ulaya ya Mashariki, au zuru duka kubwa katika Sydney.” Wafanya biashara wengi zaidi na zaidi ulimwenguni pote wanakubali yen, na baadhi yao hata wanaipendelea. “Kwa hakika, ni lazima yen ifanye maendeleo zaidi kabla ya kuchukua mahali pa dola ikiwa fedha kuu ya ulimwengu,” lasema Journal. Dola “yabaki kuwa fedha yenye hifadhi kubwa zaidi ulimwenguni” na “yaweza kutumiwa katika unamna-namna mwingi sana wa mashirika ya kifedha, na yabaki kuwa fedha ipendelewayo katika masoko ya magendo ya ulimwengu. Lakini yen inazidi kupata umaarufu upesi.”

Vyakula vya Kosha ni Afadhali?

Bidhaa zaidi ya 20,000 za kosha (vyakula vinavyotimiza viwango vya Wayahudi na Waislamu) zaweza kupatikana katika rafu za maduka makubwa ya U.S. na zinanunuliwa na wengi ambao si Wayahudi wa kidini au Waislamu shupavu (walio na sheria ileile juu ya chakula). Kwa nini? Kwa sababu watu “huhusianisha neno hilo na utakato na hali ya kufaa,” lasema Tufts University Diet & Nutrition Letter. “Lakini sheria za kosha, au ‘kashruth,’ ziliwekwa si ili kulinda afya ya mwili bali ya nafsi,” na “hilo halimaanishi nyama inayopitia ukaguzi wa kosha inakufaa zaidi ya nyama isiyo ya kosha.” Mkaguzi wa chakula Myahudi hutafuta nyama inayotimiza viwango vya lishe vipatikanavyo katika Torati, kama vile kuondoa damu, lakini yeye hajazoezwa kuchunguza kwa uangalifu ishara za uambukizo au maradhi kama vile wachunguzi wa serikali walivyozoezwa. Wala yeye hachunguzi viwango vya usafi kwenye viwanda vya utengenezaji kama vile wachunguzi wa serikali wafanyavyo, bali yeye huchunguza kwa ujumla kuona kwamba vitu vilivyochanganywa katika vyakula hivyo na mashine zapatana na sheria za kosha, ambazo “hazihusiani hata kidogo na kufaa kwa chakula mwilini.”

Watu wa Australia Wanaozeeka

Tarakimu zilizotolewa hivi karibuni na sensa ya Australia ya 1991 zilionyesha kwamba badiliko kubwa zaidi katika idadi ya watu wa nchi hiyo ni ile sehemu yenye kuongezeka ya watu wenye umri wa miaka 65 na zaidi. Ulinganisho wa sensa ya 1986 waonyesha kwamba mwendo huo ni wa jumla katika mataifa yote ya Jumuiya ya Madola. Kwa kutokeza, “asilimia ya idadi ya watoto walio na umri wa miaka 15 na chini zaidi ilipungua kutoka asilimia 23.3 hadi 22.3,” likasema gazeti The Australian. Kulingana na uchunguzi huo, umri wa wastani kwa mwanamume Mwaustralia ni 31 na kwa mwanamke ni 33.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki