Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 6/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Aluminiamu ya Kupita Kiasi
  • Chumvi Kidogo Inafaa
  • Sababu Nyingine ya Kutovuta Sigareti
  • 1991 Mwaka Ulionza Vibaya
  • Misiba ya Matetemeko ya Ardhi
  • Wanafunzi wa Dawa na Utumizi wa Dawa za Kulevya
  • Uhalifu wa Jeuri Unaongezeka Katika United States
  • Utunzi wa Afya ya Wanyama
  • Kuua au Kutoua
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1994
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1991
  • UKIMWI—Je! Nimo Hatarini?
    Amkeni!—1993
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 6/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Aluminiamu ya Kupita Kiasi

Mtaalamu wa dawa wa Toronto Dakt. Armand Lione asema kwamba katika chakula tunachokula na katika vyombo tutumiavyo kupikia huenda ikachangia machafuko ya tumbo. Yeye adai kwamba kiasi kidogo sana kama miligramu mbili au tatu za aluminiamu kikiingia kidogo kidogo katika ubongo chaweza kuvuruga utendaji wa kawaida na kutokeza namna fulani ya udhaifu. Vyombo vya kupikia, hasa wakati vitumiwapo kutayarishia au kuwekea vyakula vyenye asidi kama vile nyanya, vyaweza kuongeza kiasi cha aluminiamu, asema daktari huyo.

Chumvi Kidogo Inafaa

Kupunguza chumvi kwa kiwango cha ratli moja kwa siku kwaweza kupunguza matokeo ya ugonjwa wa moyo kwa asilimia 16 na ule ugonjwa wa moyo wa ghafula kwa asilimia 22 katika nchi za Magharibi, wanasema watafiti wa London. Kupunguza huko kwaweza kuwa na matokeo zaidi kuliko matibabu ya dawa. Wakichapisha matokeo kwenye British Medical Journal, watafiti kutoka Chuo cha Kitiba cha St Bartholomew, cha London, wanawauliza watengenezaji wapunguze kiwango cha chumvi katika utengenezaji wao. Ikiwa chumvi ingeachwa bila kutumiwa kwenye vyakula vya kutengenezwa, wanasema, ugonjwa wa moyo ghafula ungepunguzwa kwa asilimia 30 na vifo vya ugonjwa moyo wa ghafula kwa asilimia 39, ikizuia vifo 65,000 kwa mwaka katika Uingereza peke yake. Watu wanashauriwa kupunguza chumvi yao kwa kutoongeza chumvi katika meza na kuepuka vyakula vyenye chumvi nyingi.

Sababu Nyingine ya Kutovuta Sigareti

Inajulikana kwamba uvutaji sigareti unaongeza hatari ya ugonjwa wa moyo. Uchunguzi sasa unaonyesha kwamba huenda “ikazuia usumbuo unaotoa ishara ya ugonjwa wa moyo,” likasema gazeti Health, na kuondoa kusikika kwa maumivu. “Ikiwa sigareti zinazuia kusikika kwa maumivu, unaweza kuwa na umizo kubwa sana kwa moyo wako kabla ya kupata msaada wa kitiba,” asema Dakt. Michael Crawford, mwenyekiti wa Shirika la Utibabu wa Moyo.

1991 Mwaka Ulionza Vibaya

Kufuatana kwa misiba ulimwenguni pote katika miezi michache ya kwanza ya mwaka kumesonga uwezo wa mashirika ya usaidizi. “Ilikuwa tangu mwisho wa vita vya ulimwengu 2 ndipo watu wengi katika mabara mengi tofauti walipopatwa na msiba kama huo,” likasema U.S. News & World Report. Sehemu ya Urusi ya Georgia ilipatwa na matetemeko matatu. Tetemeko moja pia lilizipata Costa Rica na Panama. Vimbunga katika United States viliharibu sehemu za Kansas na Oklahoma. Tufani ya chamchela yenye pepo za mwendo wa maili 145 kwa saa moja ilipiga Bangladesh kwa muda wa saa nane, ikiuwa watu wapatao 125,000 na kuacha mamilioni bila makao. “Pamoja na uhitaji katika Ghuba na Afrika, ambapo kuna njaa inayotisha Waethiopia milioni 14 na Wasudani peke yake, misiba hii mipya imeacha mashirika yakiwa bila uwezo,” laripoti gazeti hilo. Afisa mmoja wa Chama cha msalaba Mwekundu alisema: “Sijui ni nini litakalofuata.”

Misiba ya Matetemeko ya Ardhi

Mate temeko ya ardhi yalisababisha vifo vingi mwaka jana karibu kama vile vilivyotokea katika mwongo uliopita. Kulingana na Ukaguzi wa U.S. wa Jiolojia, zadi ya misiba 52,000 kutokana na matetemeko ya ardhi iliripotiwa katika 1990, ikilinganishwa na 57,500 waliokufa kutokana na matetemeko kati ya 1980 na 1989. Huu ulikuwa msiba mkubwa sana tangu 1976. Vifo vingi vilitokea kutokana na tetemeko moja la kipimo cha 7.7 ambalo liliipiga Irani katika Juni, likiuwa watu wenye kukadiriwa kuwa 50,000 na kuumiza wengine 60,000. Ripoti hiyo iliorodhesha matetemeko makubwa ya ardhi 68 kwa mwaka uliopita, 8 zaidi kuliko mwaka uliotangulia.

Wanafunzi wa Dawa na Utumizi wa Dawa za Kulevya

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaosomea dawa wanaohudhuria Chuo Kikuu cha Texas kama vile katika Austin katika United States waliambiwa kwamba katika taifa lote, wanafunzi wanaosomea dawa wana kiwango cha juu sana cha utumizi wa dawa za kulevya kuliko shule zote za wastadi. Kwa nini? “Kwa kweli sijui,” asema msimamizi mdogo wa Chuo cha dawa Arlyn Kloesel. “Lakini ustadi unahusiana na utumizi na mwelekeo wa kuvutia aina ya mtu kama huyo. Na si yule mwanafunzi maskini. Kawaida ni yule mwanafunzi hodari, mwanafunzi kiongozi . . . ambaye hatimaye huingia matatani.” Wanafunzi walishauriwa kwamba kabla wazoevu au walevi kuweza kusaidiwa vizuri, ni lazima wakubali kwamba wana shida halafu wawe tayari kupata msaada.

Uhalifu wa Jeuri Unaongezeka Katika United States

“Uhalifu wa jeuri, mwingi ukihusiana na dawa za kulevya, unaongezeka katika kila mji wa Amerika,” lasema gazeti Newsweek. “Bunduki, kutia ndani silaha za kushambulia kivita, zaonekana ziko kila mahali—hata katika mikono ya watoto.” Mauaji yaliweka rekodi mpya mwaka jana. Watu wenye kukadiriwa kuwa 23,200 waliuawa, asilimia 60 yao kwa mabastola. “Katika kila saa 100 katika mitaa yetu sisi hupoteza zaidi ya mara tatu ya wanaume wachanga kuliko waliouwawa katika saa 100 kwenye uwanja wa vita katika Ghuba ya Uajemi,” aomboleza Mwenyekiti wa Afya na Huduma za Kibinadamu Louis sullivan. Hili ni kweli ingawa United States ina kiwango cha 426 cha wafungwa kwa idadi ya watu 100,000. Uuaji sasa ni sababisho la kifo lenye kuongoza kwa wanaume weusi kati ya umri wa miaka 15 na 24. Kwa nini uhalifu umeongezeka hivyo? Kulingana na wataalamu, “uhalifu unaongezeka wakati vithibiti vya kijamii—familia, kanisa, ujirani, na miunganisho yote isiyoonekana ya kufungamanisha jamii—huvunjika,” lasema Newsweek.

Utunzi wa Afya ya Wanyama

Dawa za wanyama wa kufugwa ulimwenguni hutia ndani kila kitu kuanzia “upasuaji wa hali ya juu hadi programu za uzuiaji wa uzito, utunzaji wa meno, na ushauri wa tabia,” laripoti The Toronto Star. “Kuwa na mnyama siku hizi ni ghali sana sana,” akasema mtunzi. Kutibu mguu wa mbwa mkubwa uliovunjika unaweza kugharimu zaidi ya dola 700 (za Kanada). Uwe tayari kulipa zaidi ya dola 800 kwa utibabu wa mchochota ini. Kupachikwa figo kwaweza kupita dola 5,000 kwa urahisi. Ushauri wa tabia hufikia dola 100 kwa saa moja. Huduma za afya ya wanyama zatia ndani wodi za kuzalia, vifaa vya utunzi wa dharura, utibabu wa kudunga visindano, elektrokadiogramu, kuondoa viziba moyo, utibabu wa meno, na hata bima ya wanyama wa kufugwa.

Kuua au Kutoua

‘Kuua kwaweza kuwa Ukristo,’ adai Kardinali wa Roma ya Katoliki Giacomo Biffi. Katika uchunguzi wa karibuni na wapingaji waaminifu Waitaliano, yeye alisma: “Unaweza kuwa Mkristo, uue, [na] ufanye vita ikiwa hilo linatumika kuokoa wengine; kama ilivyoripotiwa na gazeti la Madrid El país. Akiwa mkinzani thabiti wa utoaji mimba, alisema kwa uthabiti kwamba “amani na upingaji jeuri si viwango kamili” au hata “viwango vya Kikristo.” Askofu huyo aliambia wahudhuriaji wake waliostaajabishwa kwamba upingani mwaminifu kwa kweli ni “usio na maana” kwa sababu amani “ni taraja lisilo la kilimwengu kwamba itakuwa ndoto kuitazamia juu ya dunia hii.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki